TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

MAKALA: CHAMA CHA MAPINDUZI CCM NA UPINZANI USIOISHA NDANI YA CHAMA .


Nicholaus Kasendamila  Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Geita akitoa neno kwa wajumbe

Na Alphonce  Kabilondo,Geita 


CHAMA cha Mapinduzi CCM kiliweka msingi madhubuti ya kuchaguwa viongozi  chama kwa ngazi za mashina ,matawi , kata Wilaya na Mikoa kwa kila kipindi cha miaka mitano na kwa kutoa fursa kwa makada wote Nchini, Tanzania bara na visiwani kugombea nafasi mbalimbali za uongozi  katika jumuiya za Chama hicho UVCCM, UWT na Jumuiya ya Wazazi pamoja na chama .

Huu ni utaratibu uliowekwa na waasisi wa chama hicho akiwemo Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na wengine Sheikh Amri Abeid Karume.


 Mkoa wa Geita  ni miongoni mwa mikoa ambayo Novemba 21 mwaka huu wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM  Mkoa walikutana kwenye ukumbi wa OMEGA na kisha kuteguwa kitendawili kwa kumchaguwa Nicholaus  Kasendamila Nabaya kwa kura 464 kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho Mkoa atakae kiongoza kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2022 hadi 2027 .


Nicholaus Kasendamila ambaye kitaaluma ni mwalimu wa shule ya msingi ,pamoja na nyadhifa mbalimbali alizopitia ndani ya chama hicho aliwahi kuwa katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho miaka iliyopita Wilaya ya Geita wakati huo ikiwa ndani ya Mkoa wa Mwanza kabla ya mwaka 2012 ulipoanza rasmi mkoa wa Geita ,pia amewahi kuwa katibu mtendaji wa chama hicho katika    Wilaya kadhaa hapa Nchini .


Mwenyekiti huyo ambaye alikuwa akichuana na makada watatu akiwemo mwanasheria Wanseho Siwale ambaye ni mwanamke pekee aliyekuwa amejitosa kuwania nafasi hiyo aliyepata kura 6 kati ya kura  737 ,Alhaji Saidi Karidushi aliyekuwa akitetea kiti hicho aliibuka na kura 110 mwingine ni Daudi Sunzu Ntinonu alipata kura 126 .

Wanseho Siwale mwanamke pekee aliyejitosa kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita

 Kasendamila anakuwa mwenyekiti watatu wa chama hicho  tangu Mkoa huo ulipoanzishwa rasmi mwaka 2012 akitanguliwa na Joseph Kasheku Msukuma ,aliyekuwa mwenyekiti wa kwanza ambapo Alhaji Said Karidushi alipokea kijiti hicho mwaka 2017  . 


 Mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt Yahya Nawanda aliyekuwa msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo baada ya kutangaza matkeo hayo akatumia fursa hiyo kuwataka Viongozi waliochaguliwa kuacha tabia ya kuendeleza makundi ndani ya chama hicho .


Mwenyekiti mpya anasema kuwa katika kipindi chake cha uongozi hatarajii kuona makundi yakiendelea ndani ya chama baada ya uchaguzi  "Kumekuwepo na tabia ya watu kuendeleza makundi baada ya uchaguzi na wakati mwingine yamekuwa yakisababisha watu kutokusalimiana hii ni hatari katika kipindi cha uongozi wangu ni mraufuku" anasema Kasendamila . 


Mwenyekiti Alhaji Said Karidush aliyemaliza muda wake alisema kuwa anajivunia katika kipindi chake cha uongozi wake kuwa amefanikisha ujenzi ofisi ya chama Mkoa wakati anaingia madarakani chama haikikuwa na ofisi wala ukumbi.

Mwenyekiti Mstaafu CCM mkoa wa Geita Alhaji Said Karidushi akimtakia kila la kheri mwenyekiti mpya  CCM mkoa wa Geita mara baada ya uchaguzi kumalizika.

"Ninakukabidhi Mkoa ukiwa salaama na ofisi ya chama iliyopo mtaa wa magogo" anasema Karidushi . 

Aidha mkutano huo wa CCM Mkoa wa  ulimchagua Evarist Gervas kuwa mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (MNEC)  kwa  kura 688 kati ya kura 726 zilizopigwa aliyekuwa akitetea nafasi hiyo . 


 Makada wengine waliokuwa wamejitosa kuwania nafasi hiyo ni  Adelina Kambakama aliyeibuka na kura 20 huku Lameck akiambulia kura 14.

Mjumbe wa halmashauri kuu CCM Taifa (MNEC) mkoa wa Geita Evarist Gervas akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi mkoa wa Geita

Kada huyo Evarist Gervas alipokea kijiti hicho kutoka kwa Iddi Khassim anakuwa mjumbe wa halmashauri kuu watatu baada ya kupokea kijiti hicho kwa Iddi Kassim aliyekuwa MNEC wapili toka Mkoa huo ulipoanzishwa  mwaka 2012 akitanguliwa na Leonard Kiganga Bugomola .


Hata hivyo mjumbe wa halmashauri CCM Mkoa wa Geita kutoka Wilaya ya Mbogwe  Ngusa Charles anakiri kuwa  makambi ya uchaguzi yamekwisha, kazi kubwa kwao iliyobakia ni kufanya kazi kwa kushirikiana na kuhakikisha chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Geita kinaibuka na ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa vitongoji na Vijiji 2024 pamoja na uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka 2025.


UVCCM GEITA


Jumuiya ya umoja wa Vijana (UVCCM) mkoa wa Geita iliteguwa kitendawili hicho Novemba 16 mwaka huu kwenye ukumbi wa GEDECO Mjini Geita kwa kumchagua  Manjale Magambo kuwa mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Geita kwa kura 380 kati ya wapiga kura 415.


 Manjale aliyekuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM Wilaya ya Geita 2017 alikuwa akichuwana na makada wngine akiwemo Richard Jaba mwenyekiti aliyemaliza muda wake aliyepata kura 29.
Wengine waliochaguliwa ni mjumbe wa baraza kuu na mkutano mkuu Taifa Rubein Sagaika na Alfred Dornald mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa .


UMOJA WA WANAWAKE UWT  
Mbunge wa zamani wa jimbo la Busanda  Wilayani Geita Mkoani hapa kupitia chama cha Mapinduzi CCM Lorensia Masele Bukwimba ameibuka mshindi kwenye nafasi ya uenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi CCM (UWT) Mkoa wa Geita baada ya kuwabwaga wapinzani wake kwa kura 271 kati ya wapiga kura 315 huku Safia Bakari Mohamedi aliyekuwa akitetea nafasi hiyo akipata kura 42.
Lorensia alikuwa akitoana jasho na wagombea  nafasi hiyo ilikuwaa ikigombewa na wagombea wanne Zaituni Fundikila aliibuka na kura 2 na Mariam Walwa kura sifuri .


Wengine  ni mjumbe wa baraza kuu la Wanawake Taifa na Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Mary Mazura  aliyepata kura 296 kati ya wapiga kuraa  315 na kuwashinda wapinzani wake wawili .


Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Geita nayo ilimchaguwa  Lucas Mazinzi kwa kura 496 kati ya wapiga kura 504 zilizo pingwa Mazinzi aliyekuwa akiiongoza jumuiya hiyo toka mwaka 2017 aliyekuwa akichuwana na makada wawili Mary Mapalala kura 4 Jonathan kura 1 , pia mkutano huo ulimchaguwa Charles Kazungu kuwa Mjumbe wa baraza kuu na  Mkutano mkuu CCM Taifa .


MWISHO

Post a Comment

0 Comments