Na Urban Epimark, DODOMA.
Kamati ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya Jamii chini ya Mwenyekiti wake Mhe Stanslaus Nyongo (Mb) leo November 06, 2022 imetoa taarifa yake ya matokeo ya kikao cha kamati hiyo baina ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kilichofanyika jijini Dodoma November 04, 2022
Jengo la Ukumbi na Ofisi za Bunge, jijini Dodoma. |
Katika taarifa hiyo, kamati ya bunge imeeleza kimsingi haijaona viashiria vya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kudharau au kuonesha kiburi dhidi ya Kamati iliyoundwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolijia Mhe Dkt Adolfu Mkenda na kushindwa kutekeleza jukumu ililo agizwa bali ni mawasiliano dhaifu baina ya wizara na bodi ya mikopo.
"Kamati haijapata ushahidi wowote unaoonesha kwamba Bodi ilileta kiburi na kukwamisha utendaji wa Waziri; na baada ya adidu za rejea kuwasilishwa Bodi ya Mikopo kamati imeanza na kuendelea kufanya kazi, jambo linalo ashiria kutekelezwa kwa maelekezo ya Waziri" taarifa hiyo imeeleza.
Pia taarifa hiyo imeendelea kueleza zaidi kwamba, kuwepo kwa changamoto ya mawasiliano na mahusiano katika maeneo ya ndani ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na baina ya Wizara na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ndio chanzo cha kamati kushindwa kuanza mapema jukumu lake.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Dkt Adolfu Mkenda |
Hivyo basi kamati hiyo ya bunge imeshauri na kuelekeza changamoto zilizojitokeza zinapaswa kupatiwa ufumbuzi na serikali na kutoa mapendekezo yafuatayo:-
Mosi, mawasiliano ndani ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaboreshwe ili maelekezo ya viongozi wa sera na wasimamizi wa utekelezaji wa maelekezo ya kisera yaratibiwe kwa ufanisi na tija,
Pili, kamati iliyoundwa na Waziri iendelee kufanya kazi yake ambayo imeonekana kuwa ya tija na,
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Bw Abdul Razaq Badru. |
Tatu, Msingi wa malalamiko ya wanafunzi wa vyuo vikuu yaliyo sababisha hoja iliyo tolewa Bungeni na Mhe Eng. Ezra Chiwelesa (Mb) ni kupungua kwa bajeti ya mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza, na hivyo kusisitiza Serikali itekeleze maagizo ya Bunge ya kuhakikisha wanafunzi wote wanao stahili mikopo wanapata mikopo hiyo.
Msingi wa hoja mzima ni kuwasilishwa bungeni hoja ya malalamiko ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Vyuo Vikuu kwa mwaka huu mpya wa masomo 2022/2023 iliyo tolewa na Mhe Eng. Ezra Chiwelesa, mbunge wa Biharamulo kwamba wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanao stahili kupata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu wamekosa mikopo hiyo na hivyo kuliomba Bunge lijadili hoja hiyo.
Akitolea ufafanuzi hoja hiyo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Dkt Adolfu Mkenda katika kikao hicho alilieleza Bunge kwamba mnamo mwezi July mwaka huu aliunda kamati ya kufuatilia undani wa kusuasua kutolewa mikopo hiyo kwa wanao stahili kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu lakini kamati hiyo ilipata upinzani mkubwa na kushindwa kufanya jukumu lake.
Jengo la Utawala la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambacho ni moja ya vyuo vikuu vikubwa hapa barani Afrika. |
Mwisho.
0 Comments