Mbunge Hamis Mwagao Tabasamu (kulia) akikabidhi magodoro na blangeti kwa naibu waziri wa mambo ya ndani. |
Na Anna Ruhasha, Mwanza.
Jamii imeombwa kujitoa kusaidia makundi yenye uhitaji ikiwa ni pamoja na kutenga muda wa kujitoa kutembelea wafungwa magerezani na kutoa misaada kulingana na uwezo ili wajione hawajatengwa na jamii waliyotoka.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa mambo ya ndani Jumanne Sagini wakati akikabidhi magodoro 170 na blangeti 170 na taa za sola 3 zilizotolewa na mbunge wa jimbo la sengerema kwa wafungwa wa gereza la kasungamile wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.
Naibu Waziri akimkabidhi magodoro mkuu wa magereza mkoa wa Mwanza Justine Kaziulaya kwaajili ya Wafungwa. |
Aidha mkuu wa magereza mkoa wa Mwanza Justine Kaziulaya ameshukuru kwa Kitendo cha mbunge kujitoa kutoa sadaka hiyo na kuhidi kusimamia na kuhakikisha kila mfungwa na mahabusu wanapata.
Mbunge wa jimbo la Sengerema Hamisi Tabasamu amesema kwake siyo msaada bali ni sadaka kulingana na ombi la wafugwa kwake baada ya kutembelea gereza hilo na kukuta wanala chini ya Sakafu na kukosa blangeti za kujifunika.
Ameongeza kwa kusema kuwa yeye kama muumini aliguswa na changamoto hiyo iliyomsukuma kutumia sehemu ya msahahara wake kiasi cha zaidi ya laki nane zilizotumika kununua hao ikiwa ni magodoro ,sola na Blanketi.
“Mh waziri nilikuja katika gereza hili kama sehemu ya ziara yangu kwenye tasisi wakati naongea na wafungwa walinieleza hawana vilalio magodoro na blangeti,niliguswa maana na mimi ni binadamu naweza kuja kufungwa hapa nikamuuliza mkuu wa gereza hili jumla ya wafungwa akaniambia wapo 170 na mimi nimeleta magodoro 170 na blangeti 170 na hii ni Sedaka siyo Msaada”amesema Tabasamu.
Mbunge Tabasamu akikabidhi magodoro na Blanketi kwa Naibu Waziri Mambo ya ndani ya Nchi Jumanne Sagini kwaajili ya Wafungwa. |
Aidha , mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilayani Sengerema Maki Agustine amesema mbunge Tabasamu amekuwa akijitoa kwa jamii Hususa katika kuwaudumia wagonjwa pamoja na wafungwa siku za ijumaa kila wiki hivyo kama chama kitaendelea kumuunga mkono.
Wakati huo huo Naibu Waziri amekabidhi tofari zenye thamani ya shilingi milioni 17 kwa jeshi la polisi Sengerema zilizotolewa na mbunge Tabasamu kupitia fedha za mfuko wa jimbo kwaajili ya ujenzi wa nyumba za maaskari.
MWISHO
0 Comments