Mkurungenzi wa Halmashauri ya wilaya Sengerema Binuru Shekidele akionesha kusikitishwa na taarifa za uwongo kuhusu shule kugeuzwa danguro Sengerema. |
Na Anna Ruhasha, Mwanza.
Mkurungenzi wa halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani mwanza Binuru Shekidele amekanusha kuwepo kwa shule zinazotumika kama madanguro.
Ametoa taarifa hizo mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake siku chache baada ya baadhi ya vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kuandika habari za uwongo kuwepo kwa vyumba vya madarasa kutumika kama danguro katika halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani mwanza.
Aidha , Shekidele amesema kuwa picha za shule iliyotajwa katika mitandao ya kijamii na chombo cha kuchapisha habari hapa nchini siyo za kweli na kuwaomba wadau wa habari kuzipuuza taarifa hizo.
“ Ndugu waandishi wa habari, katika baraza la madiwani Kuliibuka hoja ya fedha za kapitesheni kifungu cha asilimia 30 ya fedha ya ukarabati na nililitolea ufafanuzi na uzuri baadhi yenu mlishiriki hicho kikao sikuzungumza kama baadhi ya vyombo vilivyochapisha, nilisema kule chifunfu kata ya madaha palikuwa na Shida ya vyumba vya madarasa kutofungwa milango lakini kwa sasa hiyo changamoto haipo baada ya kwenda kukagua na katika halmashauri yangu hakuna shule ambayo haina milango wala madirisha na chakushangaa picha za madarasa zilizotumika katika vyombo vilivyoandika uwongo siyo za hapa kwetu naomba wananchi wazipuuze ni zauwongo" amesema Mkurugenzi huyo.
Nitumie pia nafasi hii kuwaomba waandishi wa habari kufuatilia kile kinachokuwa kimesemwa ili kuondoa maswali kwa jamii hususani katika habari hiyo iliyoipotosha jamii kuhusiana na kuwepo kwa madarasa kugeuzwa madanguro wilayani hapa.
Mwisho
0 Comments