TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

PADRE SINGU AWASHUKURU WAKRISTO WAKE.

Na Urban Epimark,  GEITA

Paroko wa kanisa la Bikira Maria wa Fatima, Jimbo Katoliki la Geita Padre Gerald Singu ameishukuru Halmashauri ya Walei ya parokia hiyo kwa utumishi mzuri walio uonesha katika kipindi cha uongozi wa kanisa kwa miaka 3 iliyopita na kusema, ameonja moyo wa ukarimu na kushirikishana usio na kifani.

Padre Gerald Singu, Paroko wa Parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Jimbo Katoliki la Geita kifungua mkutano wa Halmashauri ya Walei, leo November 12, 2022

Padre Singu ambae pia ni Dekano wa Dekania ya Geita ameyasema hayo leo asubuhi November 12, 2022 alipokuwa akifungua rasmi mkutano mkuu wa Halmashauri ya Walei, Parokia ya Bikira Maria wa Fatima ambao pia ulikuwa na agenda ya uchaguzi wa viongozi wapya ngazi ya parokia.

"Nimeonja moyo wa ukarimu kutoka kwenu. Nilikuwepo na niliona ushirikiano ulio kuwepo. Na hata mlipo hitilafiana lugha mlikaa pamoja kwa upendo na kuyatatua" alieleza kwa unyenyekevu Padre Singu.

Aliendelea kuwashukuru viongozi wa Kamati Tendaji ngazi ya parokia, viongozi wa mitaa na jumuiya lakini pia viongozi wa vyama vya kitume ngazi zote kwa kujitoa kwao kufanya mambo makubwa ambayo kwa msaada wa Mungu waliweza kuyatimiza.


Sehemu ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Halmashauri ya Walei Parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Jimbo Katoliki la Geita wakimsikiliza Paroko (hayupo pichani) alipo kuwa akiongea nao katika mkutano huo.

Aliyataja mambo hayo yakiwemo ujenzi wa kanisa jipya pamoja na nyumba ya mapdre ambapo kila mmoja wetu na hata majirani wengine ni mashuhuda katika hilo kuhusu utumishi wao na kusema kwamba "msione vya elea vimeundwa"

Halikadhalika amewashukuru makatibu watendaji ngazi ya parokia kwa jinsi walivyofanya kazi yao bila kuchoka wala kulegea na pia aliwa shukuru Wahasibu au  Watunza Hazina wa parokia kwa uaminifu wao mkubwa.

Amewataka viongozi wapya na wale wa zamani wanao ondoka madarakani kufikisha pia shukrani zake kwa waamini wote wa parokia hiyo, pamoja na majirani, marafiki na wafadhili wote na pia aliwaombea kwa Mungu ili  waendelee na moyo huo wa kujitoa kulitumikia kanisa bila kuchoka.


Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Halmashauri ya Walei Parokia ya Bikira Maria wa Fatima, wakigawiwa karatasi za kupigia kura tayari kuchagua viongozi wapya leo November 12, 2022.

Mkutano huo ambao pia ulipokea baadhi ya adidu za rejea au mapendekezo ambayo Paroko Padre Gerald Singu aliuomba mkutano huo wa Halmashauri ya Walei Parokia kuyapokea na kuyafanyia tathmini jinsi ya kuyatekeleza katika kipindi cha miaka mitatu ijayo katika uongozi wao.

Pia ulifanyika uchaguzi wa kupata safu mpya ya uongozi ngazi ya Parokia ambao wataunda Kamati Tendaji ya Halmashauri ya Walei Parokia  ulio simamiwa na Mwalimu Venance Muhogo kutoka Parokia ya Nyarugusu katika jimbo hili la Geita.

Akitangaza matokeo hayo, msimamizi wa uchaguzi huo alisema jumla ya wajumbe wa mkutano huo walikuwa 75 na kumtangaza Bw Angelus Mwigune kuwa Mwenyekiti Mpya wa Parokia (kwa pindi kingine) na ambae ni Mwakilishi wa Redio Maria katika Jimbo Katoliki la Geita Bw Emanuel Mehendeka kuwa Katibu Mkuu mpya wa Parokia hiyo ya Bikira Maria wa Fatima.


Mwakilishi wa Redio Maria katika Jimbo Katoliki la Geita (Redio ya Mama) Bw Emanuel Mehendeka (pichani) amechaguliwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Halmashauri ya Walei Parokia kuwa Katibu Kuu wa Parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Jimbo Katoliki la Geita leo November 12, 2022

Viongozi wengine walio chaguliwa ni pamoja na Bw George Claver katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti na Bw Francis Kazaula kwa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Parokia.

Nafasi ya Wahasibu au Waweka Hazina imekwenda kwa Mama Ester Punguka, ambae atakuwa Mhasibu Mkuu na Mama Elizabeth Mhando atakuwa Naibu wake. 

Majina ya viongozi hao yamepelekwa kwa Baba Paroko na Msimamizi wa Uchaguzi kwa kuyathibitisha na endapo ataridhia atayatangaza yeye rasmi kuwa viongozi wapya wa Kamati Tendaji ya Halmashauri ya Walei Parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Jimbo Katoliki la Geita.


Safu mpya ya uongozi wa Kamati Tendaji ya Halmashauri ya Walei Parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Jimbo Katoliki la Geita wakiwa wamesimama mbele ya wajumbe walio wachagua muda mfupi baada ya Msimamizi wa Uchaguzi huo kuwatangaza. Aliye simama nyuma yao (mwenye Kaunda Suti Nyeusi) ni Msimamizi wa Uchaguzi huo, Mwalimu Venance Muhogo kutoka Parokia ya Nyarugusu, Jimbo Katoliki la Geita leo November 12, 2022.

Kulingana na utaratibu wa Katiba ya Halmashauri ya Walei, chini ya usimamizi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania-TEC, viongozi wake hudumu kwa kipindi cha miaka mitatu katika uongozi  kisha wana chaguliwa tena, na hawa wa sasa wata hudumu kuanzia mwaka 2023 hadi 2026.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments