Pichani anaesoma aliyevaa suti nyeusi ni Ndositwe Haonga Mkurugenzi wa mambo ya ndani TRA Nchini ,muwakilishi wa mkurugenzi wa TRA Nchini.
Alphonce Kabilondo na Samwel Masunzu ,Geita
Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigela ameitaka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Geita kuweka mazingira rafiki ya ukusanyaji wa mapato ili kuleta ufanisi mkubwa katika ukusanyaji wa mapato kwa wafanyabiashara Mkoani humo .
Mkuu huyo amesema hayo mjini Geita wakati akitoa vyeti kwa walipa kodi waliofanya vizuri kwa kulipa kodi bila shuruti mkoani Geita.
Shigela alisema kuwa serikali kufikia malengo yake lazima kuwepo na mazungumzo na wafanyabiashara pamoja na kuwapatia elimu badala ya kutumia nguvu katika kukusanya mapato.
Shigela akisistiza kauli hiyo alisema mamlaka hiyo haina budi kuweka mazingira rafiki ya ukusanyaji wa mapato ili kuweza kuleta ufanisi mkubwa katika kukusanya mapato.
Aidha Ndositwe Haonga akizungumza kwaniaba ya Kamishina wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA alisema, kupitia elimu ambayo wamekuwa wakiitoa kwa wafanyabiashara, kila mara imeonyesha mafanikio makubwa yameonekana kwenye ukusanyaji wa kodi .
Ndositwe alisema kuwa mamlaka hiyo imejipanga kuboresha matumizi ya mashine za kielektroniki na ujenzi wa vituo vya TEHAMA kusajiri walipa kodi na kubuni vyanzo vya mapato .
Akizungumzia changamoto alisema kuwa baadhi ya wafanyabiashara wasio waadilifu hawatumii mashine za kielektroniki kwa usahihi pamoja na kutotoa risiti hali ambayo inachangia serikali kupoteza mapato
Meneja wa mamlaka hiyo Mkoa wa Geita Hashim Ngoda alisema kuwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 walikusanya asilimia 97% na kwa kipindi cha Julai hadi Oktoba 2022 wamefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 25 sawa na ufanisi wa asilimia 208% huku lengo likiwa nikukusanya bilioni 35 kwa mwaka 2022/2023 .
Baadhi ya wafanyabiashara waliopatiwa vyeti hivyo akiwemo, Mkurugenzi wa Blue Coast Investement Bw, Athanas Inyasi wameishukuru serikali kupitia TRA kwa kutoa motisha kwao ambapo wameahidi kuendelea kulipa kodi bila shuruti .
Wakati huo huo katika kuadhimisha wiki ya mlipakodi, Mamlaka ya mapato TRA mkoani Geita imetoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Nyankumbu Girls ,na msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vifaa vya shule daftari ,Sabuni miswaki , mafuta ya kujipaka Unga ,Mchele kwenye vituo vya watoto wenye mahitaji maalumu vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya milioni 6.
Mkuu wa shule ya sekondari Nyankumbu Girls Jojia Mgashe akipokea msaada huo alisema kuwa shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya elfu moja huku Sista Maria Lauda wa kituo cha Moyo wa Huruma kinachomilikiwa na kanisa katoliki akitumia fursa hiyo kuipongeza TRA Mkoa wa Geita .
MWISHO.
0 Comments