Anna Ruhasha, Mwanza . Meneja wakala wa ufundi Tamesa mkoa wa mwanza Alyoce Ndunguru akitoa taarifa ya ujenzi mpya wa kivuko cha nyakalilo Kome
Taarifa hizi zimetolewa na meneja wakala wa Ufundi ( Tamesa )mkoa wa mwanza Alyoce Ndunguru …wakati akikabidhi kivuko cha mv Sabasaba kwa wakazi wa kome ili kupunguza adha ya kutumia kivuko kimoja cha mv komeII ambacho ndicho kilikuwa kikitumika
“Tunafahamu wakazi wa kome kiu yenu ni kuona kivuko kipya lakini kulingana na uhitaji na ombi la mbunge tumeona kwanza tulete kivuko hiki cha mv sabasaba japo siyo kipya lakini kimefanyiwa matengenezo na maboresho lakini pia nikikubwa kuzidi hiki cha mv kome II na hii itapunguza changamoto za kubanana kwenye kivuko kimoja kama hilivyokuwa hapo nyuma na vikuko vyote vitafanya kazi “amesema
Baadhi ya viongozi walioshiriki katika mapokezi ya kivuko cha mv sabasaba kabaganga |
Aidha ametumia muda huo kuwaomba wananchi kutunza miundombinu ya vivuko hivyo kutoka na serikali kutumia fedha nyingi kuvitengeneza.
Baadhi ya wakazi wa kisiwani kome ,Ajelina kyaruzi na Johnsen licha ya kupongeza mbunge kuanza kutimimiza baadhi ya ahaadi zake wasema kuwa kilio chao kikubwa nikuona kivuko ambacho watasafiri pasipokuwepo na changamoto za
kunyeshewa mvua na kusafiri wamesimama.
“Tulipo ambiwa tunaletewa kivuko tuliamasika kuja kama unavyotuona lakini mioyo yetu imesononeka kwasababu kivuko hiki hakina tofauti na mv komeII ambayo tunaitumia labda ukubwa tu,sisi hatutaki vivuko vya mifugo tunataka vivuko kama vilivyo vya Busisi ‘wakati wa mvua na jua tuwetuna safiri kwa raha” wamesema.
Akizungumza na mamamia ya wakazi wa kome Mbunge wa jimbo la Buchosa Erick
Shigongo amewaondoa ofu wapiga kura wake na kusema anajua huitaji wao wa kivuko kipya wakati wakisubiri miezi 24 kukamilika kivuko kipya ameona alete mv sababa.
Baadhi ya wananchi walioshiriki |
“Mimi ni miongoni mwa watu waliozaliwa na kukulia katika maisha ya chini sana najua sana kwanini nimeamuao kutanguliza hiki kivuko ,kivuko ni sehemu ya haadi zangu lazima kivuko kipya kije tena kikubwa na serikali imeishamlipa..,,bilion mbili,ninacho waomba tupendane tushirikiane tuijenge Buchosa yetu"
Katika hafla hiyo mkuu wa wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga ambaye alikuwa mgeni rasmi amewataka wasimamizi wa vivuko hivyo kwenda na muda na kuhakisha wanasafirisha wananchi kwa muda ili Pangea na siyo kuwakalisha vituoni.
Mbunge wa jimbo la Buchosa Erick Shigongo akizungumza na wakazi wa Buchosa. |
Hata hivyo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mack Agustine makoye Dm ameongeza kuwa chama kitaendelea kuwapatia ushirikiano viongozi wanaotokana na chama hicho hasa wanaosukuma maendeleo kwa wananchi.
“Chama hakijalala tutawapa ushirikiano viongozi wetu,lakini pia niwaonye mnaonza kampeni chini chini kuna wengine wanagawa baiskeli kwaajiri ya ubunge ,mimi ndiyo mwenyekiti sitawafumbia macho,acheni watu wafanye kazi siyo manenomaneno”amesema Dm.
Picha ya kivuko kipya |
Mwisho
0 Comments