Na Urban Epimark, DAR ES SALAAM.
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji ameitaka Bodi ya Wakurugenzi ya GS1-TANZANIA kujadili fursa za kuwawezesha watu kiuchumi kupitia mifuko ya fedha na mikopo kwa wazalishaji wa bidhaa nchini inayo patikani katika wizara hiyo.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt Hashil T. Abdallah kwa niaba ya Waziri Dkt Ashatu Kijaji kwenye mkutano mkuu wa 11 wa mwaka wa GS1-TANZANIA uliofanyika jijini Dar es Salaam jana November 29, 2022.
"Serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na GS1-TANZANIA katika kuwapatia leseni za Barcodes wazalishaji wa bidhaa zinazo zalishwa nchini lakini pia kuzitangaza katika masoko ya ndani na kimataifa, lakini wanapitia changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mitaji" alisema Naibu Katibu Mkuu.
Naibu Katibu Mkuu huyo aliendelea kueleza mbele ya wanachama wa GS1-TANZANIA katika mkutano huo kwamba, wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara zipo fursa zaidi ya 62 za mifuko ya fedha za kuwezesha watu kwa njia ya kukopesha ili kupata mitaji lakini fursa hizo hazifahamiki na hivyo kuitaka Bodi ya GS1-TANZANIA kuweka agenda ya kuzijadili hilo katika mkutano huo na kisha kupeleka ripoti wizarani, alisema zaidi Naibu Katibu Mkuu.
Akitoa salamu za shukrani kwa serikali zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan na pia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Dkt Hassan Ally Mwinyi kwa kuwezesha mazingira mazuri ya kuzalisha na kuuza bidhaa ndani na nje ya nchi, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya GS1-TANZANIA Prof Mohamed Khalfan alisema tatizo linalo wakabili wazalishaji wengi nchini ni ukosefu wa mitaji.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya GS1-TANZANIA Bw Jumbe Menye kwenye taarifa yake katika mkutano huo mbele ya Mgwni Rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara alisema,
"GS1-TANZANIA kwa kipindi cha miaka 3 iliyopita, iliathiriwa shughuli zake na mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO-19 na hivyo mipango mingi ya bodi hiyo kushindwa kutekelezeka" alisema.
Mwenyekiti wa Bodi ya GS1-TANZANIA Bw Jumbe Menye akiwasilisha taarifa yake ya shughuli za Bodi hiyo katika mkutano huo November 29, 2022. |
Sababu nyingine ni kutetereka kwa mifumo mbalimbali ya kufanikisha Biashara nchini ili shughuli za GS1-TANZANIA katika kutoa leseni za Barcodes ziwe rahisi ikiwemo mifumo ya fedha kwenye mabenki na pia upande wa TEHAMA.
Katika mkutano huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1-TANZANIA Bi Fatma Kange akisoma maazimio tisa yaliyo pendekezwa kutekelezwa kuanzia mwakani 2023 ili kuimarisha shughuli za utoaji leseni za Barcodes nchini, ofisi zaidi za kutoa huduma hizo zitaanzishwa kila mkoa na pia ushirikiano zaidi baina ya taasisi za umma zikiwemo SIDO na TBS zitaimarishwa zaidi.
Mwisho.
0 Comments