Na Urban Epimark, GEITA.
Umoja wa Wanaume Wakatoliki Tanzania (UWAKA) ngazi ya Parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Jimbo Katoliki la Geita leo wamewapata viongozi wapya watakao simamia na kuongoza umoja huo kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2023 hadi 2026.
Parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Jimbo Katoliki la Geita. |
Uchaguzi huo ambao ni muendelezo wa chaguzi za Halmashauri ya Walei kiparokia katika Jimbo, chini ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania-TEC unajumuisha pia viongozi wa vyama vingine vya kitume pamoja na wale wa Jumuiya ndogo ndogo, ulifanyika leo kwenye kumbi za Parokia ya Bikira Maria wa Fatima mjini Geita.
Msimamizi wa uchaguzi huo Katekista Simon Pauline aliwaambia wajumbe wa mkutano huo ulioshirikisha wawakilishi kutoka mitaa 7 kati ya 10 ya parokia hiyo na pia kigango kimoja kati ya viwili vilivyopo kwamba,
"Uchaguzi wa viongozi wa vyama vya kitume pamoja na jumuiya ndogo ndogo huwa kampeni haifanyiki bali ni kwa kupitia sala na maombi kwa Mungu Roho Mtakatifu ambae kwa uweza wake huwachagua viongozi wa Walei kuwaongoza" alisema.
Mkutano huo wa uchaguzi ngazi ya parokia hiyo, ulioenda sambamba na chaguzi za vyama vingine vikiwemo Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA), Vijana Wakatoliki Tanzania (VIWAWA), Chama cha Lejio Maria na kile cha Wazee Wastaafu cha Mt Augustino.
Mwenyekiti aliye chaguliwa kuiongoza UWAKA, Parokia ya Bikira Maria wa Fatima Bw Salvatory Kazaula (aliye tetea nafasi yake) aliwashukuru wana UWAKA wote kwa kutimiza wajibu wao wa kuchagua uongozi mpya ngazi ya parokia na kusema hiyo ni nguvu mpya.
"Namshukuru sana Mungu leo kwa kutupatia viongozi wapya wa UWAKA ngozi ya parokia kwani tuna amini ni kwa uweza wa Mungu mwenyewe. Kuanzia leo UWAKA haitabaki tena nyuma kwa kazi za kitume hivyo tufungue ukurasa mpya kiutendaji" alisema Mwenyekiti wa UWAKA.
Nae Katibu Mkuu mpya wa UWAKA aliye chaguliwa ambae anatokea Mtaa wa Msalala Road Bw Beatus Mazezere aliwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa UWAKA kwa imani yao walio onesha kwake hadi kumchagua na kutoa ahadi kwa Mwenyekiti wa UWAKA wa Parokia hiyo Bw Salvatory Kazaula kwamba atafanya kazi kwa bidii na kujituma ili kuhakikisha UWAKA inasonga mbele.
Uchaguzi mkuu wa viongozi wa Kamati Tendaji ya Halmashauri ya Wakei Parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Jimbo Katoliki la Geita unatarajiwa kufanyika jumamosi ijayo November 12, 2022 na viongozi wa vyama vya kitume waliochaguliwa leo wakiwemo UWAKA ni wajumbe wa mkutano huo wa uchaguzi.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa UWAKA ngazi ya Parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Jimbo Katoliki la Geita wakiwa kwenye ukumbi tayari kwa uchaguzi leo November 05, 2022 |
Mwisho.
0 Comments