Na Mwandishi wetu, Dodoma.
Makamu wa Rais wa Muungano wa klabu za waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Pendo Mwakyembe ametoa wito kwa viongozi wa Klabu zote za Waandishi wa habari kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kubuni vyanzo vya mapato ili kuweza kuwa na Klabu imara zenye tija kwa wanachama wake, jamii na taifa kwa ujumla.
Amebainisha hayo wakati akifungua mafunzo ya uongozi na usimamizi wa fedha kwa viongozi wa klabu kutoka mikoa ya Geita, Kigoma, Kagera, Mara, na Simiyu yanayoendelea jijini Dodoma kwa siku tatu mfurulizo kuanzia leo November 2 hadi 4,2022 lengo ni kuwaongezea ujuzi na maarifa ya Uongozi na Usimamizi wa fedha ili kuleta ufanisi wa kiutendaji katika Klabu zao ili kuendana na Kasi mpya ya UTPC inayongozwa na kauli mbinu isemayo "Moving UTPC from good to great" .
Amesisitiza viongozi wa ngazi za juu katika Klabu wanapaswa kuwa na mshikamano na mahusiano mazuri wao wenyewe kwanza na kisha kwa wanachama wao wote huku wakizingatia miongozo ya UTPC ili Klabu zisiwe kikwazo kwa wafadhili mbali mbali wenyenia ya kufanya kazi na Waandishi wa Habari Tanzania.
"Kiongozi yeyote wa Press Club asiyeweza kubuni walau chanzo cha mapato ndani ya muda wa kipindi cha miezi mitatu au mitano, anapaswa kujitathimini kwakweli” alisema Mwakyembe.
"Niwaombe Viongozi wa Klabu zote tubadilike kifikra, Let's move from Comfort zone katika utendaji ili tuboreshe ufanisi wa klabu zetu na UTPC kwa ujumla” alieleza Maleko.
Akichangia mawazo yake kwa niaba ya washiriki wa Mafunzo haya Renatus Masuguliko ambaye ni Mwenyekiti wa Geita Press Club-GPC aliipongeza UTPC kwa kuendesha mafunzo hayo na kwamba yatasaidia kuimarisha mifumo ya uongozi na Usimamizi wa fedha, mambo ambayo yamekuwa chanzo cha migogoro mingi ya klabu nyingi hapa nchini.
"Mafunzo haya nimazuri sana, tunaahidi kubadilika kwani mambo mengine tulikuwa hatujui na baadhi yetu nimafunzo ya mara ya kwanza" alisema Masuguliko.
Mwisho.
0 Comments