Rais Samia akitoa Tuzo kwa muasisi wa kanisa la Waadventista Wasabato wa mkoa wa Dodoma leo November 19, 2022 |
Na Urban Epimark, DODOMA.
Kanisa la Waadventista Wasabato wa mkoa wa Dodoma leo limeadhimisha Jubilee ya miaka 50 ya Utume na Huduma tangu kuanzishwa kwake na kumwomba Rais Samia awasaidie kuondoa changamoto tatu kubwa zinazo wakabili.
Rais Samia ambae alikuwa Mgeni Rasmi katika Jubilee hiyo, kanisa hilo limemweleza changamoto za kubinywa uhuru wao wa kuabudu siku za jumamosi ambapo waamini wao hushindwa kuhudhuria usahili wa ajira na mitihani siku hiyo na hivyo kuzikosa fursa za ajira zinazo tolewa.
Rais Samia Suluhu Hassan akikaribishwa na chipukizi wa Kanisa la Waadventista Wasabato katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma kwa kupigiwa salute ya heshima leo November 19, 2022 |
"Mhe Rais, kanisa la Waadventista Wasabato linazo changamoto tatu kubwa kwa wafuasi wetu kukosa nafasi za ajira serikalini na kwingineko kwa vile waandaaji wa usahili hupanga kuwaita wasahiliwa siku za jumamosi ambapo ni siku yetu ya kumwabudu Mungu" ilisema sehemu ya taarifa ya kanisa hilo iliyosomwa mbele ya Rais Samia leo katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Changamoto zingine ni kutoheshimika siku ya Jumamosi ambayo ni siku rasmi ya Wasabato kuabudu na kumtukuza Mungu kama ilivyo kwa madhehebu mengine ya wakristo na waisalamu siku zao zinaheshimika na pia kuomba kupatiwa wataalamu wabobezi wa tiba ya afya kwa hospitali zao.
Katika hotuba yake aliyoitoa na kurushwa moja kwa moja na vyombo vya habari leo asubuhi November 19, 2022 kutoka jijini Dodoma, Rais Samia ambae alikuwa Mgeni Rasmi katika Jubilee hiyo alilishukuru kanisa hilo kwa jinsi wanavyoiasaidia serikali katika malezi ya watoto na vijana hapa nchini na kusaidia kudumisha maadili ya utamaduni pamoja na mila za kitanzania.
Halikadhalika Rais Samia ameutaka uongozi pamoja na maaskofu wa kanisa hilo halikadhalika viongozi wote wa madhehebu mengine ya dini hapa nchini kufikisha ujumbe kwa wafuasi wao wa kutunza mazingira kwa kupanda miti na kuitunza ili kurejesha uoto wa asili na kusaidia upatikanaji wa maji na mvua za kutosha za misimu.
Awali akimkaribisha Rais Samia ili azingumze na wafuasi wa kanisa hilo walio furika katika ukumbi wa Jakaya Kikwele jijini Dodoma, Askofu Mkuu wa Jimbo la Kaskazini wa Kanisa hilo Askofu Mark Marekana alimshukuru Rais Samia kwa Upendo na Ukarimu wake kwa watanzania kwa kuimarisha kwa kiwabgo cha juu huduma za Elimu na Afya hapa nchini pamoja na ujenzi wa miundombinu mingine ikiwemo madaraja na viwanja vya ndege.
Pia Askofu huyo alimwombea kheri nyingi Rais Samia katika uongozi wake kwani Tanzania imeshuhudia kuwa na Amani na Ushirikiano mkubwa baina ya watanzania na majirani zake wote na kutoa ahadi kwamba kanisa hilo litaendelea kutoa ushirikiano kwake kwa muda wote.
Kanisa la Waadventista Wasabato liliaaza rasmi hapa nchini mwaka 1903 katika wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro na kuenea kidogo kidogo kuelekea Musoma mkoani Mara na kufika hadi mkoani Dodoma kunako mwaka 1972 ambapo leo ndio maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50 ya Utume na Huduma katika mkoa wa Dodoma.
Rais Samia akiondoa kitambaa kama ishara ya kuzindua ujenzi wa Mnara wa Jubilee ya miaka 50 ya Utume na Huduma ya kanisa la Waadventista Wasabato wa mkoa wa Dodoma leo November 19, 2022 |
Mwisho.
0 Comments