TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

BINTI MBARONI KWA KUZIKA MTOTO WAKE AKIWA HAI ILI AKALE BATA

Kamnda wa jeshi la polisi Mkoa wa Geita ACP  Safia Jongo

Na Alphonce Kabilondo,Geita .

Binti Mmoja  Oliva Meshack 19 mkazi wa Mapinduzi kata ya Buseresere  wilayani  chato Mkoani Geita anadaiwa kumuawa  mototo wake mchanga wa umri wa  siku 14 kwa kumfukia  kwenye shimoni kwa  madai ya ugumu wa maisha .

Kwamujibu wa kamanda wa  jeshi la polisi Mkoa wa  Geita kamishinina msaidizi wa jeshi la  polisi ACP Safia Jongo amesema kuwa tukio hilo limetokea disemba 9 mwa huu baada kijijini .

Kamanda huyo alisema kuwa  Binti huyo alimfukia shimoni mtoto wake na kisha kusababisha kifo cha mtoto wake bila huruma ili aweze kupata muda wa kwenda kula bata (kudanga) .

Tulipata taarifa kutoka kwa raia wema  kuwa kuna binti huko Buseresere Wilayani Chato alikuwa amejifunguwa mtoto kwa sasa  mtoto huyo haonekani jeshi la polisi lilianza uchunguzi baada ya kumtia mbaroni Binti huyo alikiri kumfukia mtoto wake shimoni na ili apate muda wa kufanya biashara ya ngono akidai kuwa ana maisha magumu kwasasa jeshi la polisi linamshikilia”alisema kamanda Jongo .

 Aidha katika tukio jingine Mchungaji mmoja ambaye kanisa lake halijafahamika Abduel Raphael  (42)  Mkzi wa Mtaa wa Uwanja kata ya Nyankumbu Wilayani Geita Mkoani hapa amefariki dunia kwa njaa  baada ya kufunga maombi maalumu kwa muda wa siku nane akidai kuwa ikitoea akafariki dunia atafufuka .

Tulipokea taarifa disemba 9 mwaka huu kutoka kwa mwenyekiti wa Mtaa wa Uwanja Enos Charahani kuwa kuna Mchungaji amefariki dunia akiwa kwenye maaombi baada ya jeshi la polisi kufika walikuta mwili wake umeharibika huku ukitoa harufu na baada ya uchunguzi kufanyika tulibaini chanzo ni njaa “alisema kamanda Jongo .

Kamanda huyo amefafanuwa kuwa Mchungaji huyo alikuwa akiishi nyumbani kwa Leonard John Mtaa wa Uwanja kata ya Nyankumbu Mkoani hapa na kwamba alikuwa akiwaaminisha waumini wake kuwa anauwezo wa kufa na kufufuka na kufunga bila kunywa wala kula chochote .

Ameongeza kuwa mwenye uwezo wa kufa na kufufuka alikuwa ni Yesu Kristo peke hakuna mwingine tena hapa duniani .

MWISHO

Post a Comment

0 Comments