TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

GEITA PRESS CLUB YABISHA HODI OFISI YA MKUU WA MKOA DODOMA

 Mkuu wa Mkoa Dodoma Rosemary Senyamule (katikati)akipokea hati ya pongezi kutoka kwa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Geita, kushoto ni Renatus Masuguliko Mwenyekiti GPC akimkabidhi hati ya pongezi kwa niaba ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Geita na upande wa kulia ni Novatus Lyaruu Katibu Mkuu Mtendaji wa shughuli za kila siku za Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Geita aliyeambatana na Mwenyekiti GPC jijini Dodoma. 

Na Mwandishi wetu,Dodoma. 

Leo tarehe 19 Disemba 2022 viongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Geita (GPC) wamefika katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, kumpatia hati ya pongezi ya kutambua mchango wake katika kuleta maendeleo ya mkoa wa Geita wakati akiwa Mkuu wa mkoa huo kabla ya kuhamia Dodoma, hati  hii imetolewa na chama cha waandishi wa habari mkoa wa Geita (Geita Press Club-GPC) na imekabidhiwa kwake na Viongozi wa ngazi za juu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Geita  (Geita Press Club-GPC).

Mkuu wa Mkoa Dodoma Rosemary Senyamule akiwatayari kupokea hati ya kumpongeza kwa kazi nzuri kutoka kwa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Geita. 

Hata hivyo katika kujenga na kukuza mahusiano viongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Geita Renatus Masuguliko (Mwenyekiti GPC) na Novatus Lyaruu (Katibu Mkuu Mtendaji GPC) walitembelea Ofisi ya Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma ambapo waliambatana nao hadi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma walipokuwa wakielekea ili kukabidhi hati ya pongezi Mkuu huyo wa Mkoa ambe awali alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kabla ya kuhamishiwa Dodoma. 

Mwenyekiti wa Geita Press Club-GPC Renatus Masuguliko (Kushoto) alieleza azma ya Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Geita kuamua kumpatia hati ya kumpongeza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule ambaye kwa sasa ndiye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Novatus Lyaruu (Kulia) aliyeambatana na Mwenyekiti huyo jijini Dodoma. 

Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule (Aliyenahati), kulia kwake ni Mussa Yusuf (Mwenyekiti Dodoma Press Club) akifuatiwa na Renatus Masuguliko (Mwandishi wa Habari Mwandamizi Mwenyekiti wa Geita Press Club-GPC), upande wa kushoto kwake ni Novatus Lyaruu (Katibu Mkuu Mtendaji GPC) akifuatiwa na Ben Bango (Katibu Mkuu Mtendaji wa Dodoma Press Club) wakiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma leo 19 Disemba 2022.

Novatus Lyaruu Katibu Mkuu Mtendaji GPC akiwa katika picha na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule. 


Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments