TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

GS1-TANZANIA INAKUJA KIVINGINE MWAKA 2023

Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1-TANZANIA Bi Fatma Kange.

Na Urban Epimark, DAR ES SALAAM 

Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa GS1-TANZANIA Bi Fatma Kange ameishukuru Bodi ya Wakurugenzi ya taasisi hiyo  pamoja na uongozi wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha inafikia malengo ya juu katika kuwahudumia wanachama wake hapa nchini.

Mbali na athari za mtikisiko wa uchumi kutokana na ugonjwa wa UVIKO-19 takribani miaka mitatu inapita sasa, CEO amesema mipango mingi ilisimama lakini sasa GS1-TANZANIA imejipanga  kurejea kivingine kutoa huduma zake zenye tija zaidi  kuanzia January 2023.

Kwa upande wa watendaji wa GS1-TANZANIA, Bi Fatma Kange  ametoa rai kwao kujiandaa kwa utendaji mpya wenye kasi, kujituma zaidi na kuwa  wabunifu ili kufanikisha malengo au maazimio ya mkutano mkuu huo wa mwaka wa wanachama.

Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1-TANZANIA Bi Fatma Kange akiwa katika picha na baadhi ya watumishi wa taasisi hiyo.

"Naomba watumishi tubadilike tuendane na kasi ya sasa inavyo hitaji Bodi yetu lakini pia tuoneshe shukrani kwa jinsi serikali kupitia Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ilivyo tuunga mkono katika kusaidia kutatua changamoto zilizopo" amesema Bi Fatma Kange.

Mwakani 2023, GS1-TANZANIA imepanga kutekeleza maazimio tisa ambayo yamelenga kuimarisha upya huduma zake kwa wazalishaji na wahitaji wa leseni za Barcodes hapa nchini ikiwemo kutambulisha mfumo mpya wa utoaji leseni hizo kwa njia ya kielectroniki.

Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1-TANZANIA Bi Fatma Kange (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha na baadhi ya wazalishaji wamiliki wa leseni za Barcodes hapa nchini.

Mpango mwingine ni  kuimarisha zaidi mahusiano yake na wizara za serikali, taasisi za umma zikiwemo TIRDO, TBS, SIDO, NEEC, LGA na zingine nyingi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1-TANZANIA Bi Fatma Kange (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya watumishi wa GS1-TANZANIA katika picha baada ya kumalizika kwa AGM-2022 jijini Dar es Salaam.

Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments