TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

JAMII FORUMS YAZINDUA USHIRIKIANO NA UMOJA WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA

Katika picha upande wa kushoto ni Bw.Keneth Weston Simbaya (Mkurugenzi Mtendaji UTPC) na kulia ni Maxence Melo (Mkurugenzi  Mtendaji Jamii Forums) wakisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati wa Taasisi wanazoongoza. 

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam 

UTPC na Jamii Forums wameingia katika Ushirikiano wa Kimkakati kwa lengo la kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari Nchini katika kuandaa Habari za Kiuchunguzi (IJ) na zenye Maslahi ya Umma (PIJ) ili kuchochea Uwajibikaji na utawala bora. 

Bw. Keneth Weston Simbaya (Mkurugenzi UTPC) na Maxence Melo Mkurugenzi wa Jamii Forums (Suti nyeusi) wakionesha hati ya makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati baada ya kusaini. 

Pia, Waandishi watajengewa uwezo kuhusu Usalama wa Kidijitali, matumizi sahihi na bora ya Vifaa na Mifumo ya Kidijitali na namna bora ya kutumia Uwanja wa Kidijitali kuendeleza kazi zao. 

Aidha, Mkurugenzi wa JamiiForums amesema litaanzishwa shindano la #StoriesOfChange litakalowalenga waandishi wa habari na washindi watatuzwa baada ya mchujo. 

Ushirikiano huu ni miaka 2, utaanza rasmi Januari 2023 na unaweza kuhuishwa baada ya kufanya tathmini. 

Pichani wakwanza kutoka kulia ni Victor Maleko (Afisa Program Machapisho, Utafiti na Mafunzo UTPC) katikati ni Mkurugenzi wa Jamii Forums Maxence Melo akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji UTPC Bw. Keneth Simbaya. 

#JamiiForums #InvestigativeJournalism #JFUwajibikaji #DigitalRights

Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments