TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

MEDIA ENDELEENI KUWA CHACHU YA MAENDELEO GEITA.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Wilson Shimo akifungua mkutano maalum wa klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Geita (Geita Press Club) uliofanyika ukumbi wa Bwalo la Polisi mjini Geita leo December 22, 2022.

Na Urban Epimark,  GEITA.

Imeelezwa kwamba uwepo wa wanahabari kupitia vyombo vyao wanaofanya kazi zao kwa usahihi na kwa kuzingatia maadili na miiko ya uandishi katika mkoa wa Geita, kumekua chachu ya kuongeza hamasa ya wananchi kutamani kufikia maendeleo yao na hivyo kubakia kuwa nyenzo muhimu ya kuleta maendeleo ya watu.

Halikadhalika usahihi na muda muafaka wa kuwasilisha taarifa mbalimbali za kijamii ikiwemo kero za watu na kuibua maovu, kumesaidia viongozi wengi wa serikali kuelewa changamoto zinazo wakabili wananchi na kuzishughuliakia kwa wakati,  hivyo wanahabari ni nyenzo muhimu sana kwa jamii.

Haya yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Wilson Shimo leo December 22, 2022 wakati alipokuwa Mgeni Rasmi kwenye Mkutano Mkuu maalum wa klabu ya waandishi wa habari ya mkoa wa Geita (Geita Press Club-GPC) uliofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Jeshi la Polisi mjini Geita.

Baadhi ya wanachama wa klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Geita (Geita Press Club-GPC) wakimsikiliza Mgeni Rasmi latika mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Wilson Shimo (hayumo pichani) wakati akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika Bwalo la Polisi mjini Geita leo December 22, 2022

"Nawapongeza sana waandishi wa habari wa hapa wilayani Geita na hata kwenye mkoa wetu mzima wa Geita. Mmekuwa mkifanya kazi nzuri na kwa usahihi mkubwa japo kuna changamoto zinazo wakabili ikiwemo kukosa gharama za usafiri kuwafikisha kwenye matukio, lakini hamjakata tamaa na wala hakuna migogoro inayo ibuka baina yenu na jamii kwa habari mnazo ripoti, hongereni sana" alisema Mkuu wa Wilaya.

Rai yangu kwenu muendelee kufanya kazi zenu kwa usahihi na kwa kuzingatia miiko na maadili ya uandishi wa habari.

Mwandishi wa Habari kutoka Uhuru Publications (Uhuru Digital) Bi Rose Mweko (mwenye miwani kushoto) pamoja na waandishi wengine wa habari ambao ni wanachama wa klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Geita (Geita Press Club) wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Wilson Shimo (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano huo mjini Geita leo December 22, 2022.

Pia amewataka wanahabari wajitahidi kuongeza viwango vyao vya taaluma ili wasibakie nyuma ili waendelee kuwa tegemeo kwa jamii nzima.

Nae mwakilishi wa jeshi la polisi katika mkoa wa Geita ambae amemwakilisha Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Geita katika mkutano huo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Thomas Joseph amesema,

Mrakabu Mwandamizi wa Polisi katika mkoa wa Geita Afande Thomas Joseph ambae katika mkutano huo alimwakilisha RPC wa Mkoa wa Geita ambae alialikwa katika mkutano huo lakini akaoata udhuru wa kikazi kuwa nje mkoa, akitoa salamu na ujumbe wa jeshi la polisi kuhusu wananchi kudumisha amani wakati wa sikukuu za Chrismas na Mwaka katika mkutano huo.

"Hali ya usalama ya wananchi pamoja na mali zao katika mkoa wa Geita ni salama na kuna utulivu mkubwa katika jamii na wananchi wanaendelea vyema na shughuli zao kuelekea kwenye sikukuu za msimu wa Chrismas na Mwaka Mpya 2023" alisema.

Afisa huyo wa polisi aliendelea kueleza zaidi kwa kutoa wito kwa wananchi kwamba, wachukue taadhari na kuwa makini wanapo sherekea sikukuu, wasijisahau kuacha makazi yao bila ulizi wowote ili kuepuka ualifu unaoweza kujitokeza ikiwemo wizi wa mali na wadokozi wengine.

Kamanda wa TAKUKURU katika wilaya ya Geita Bw Said Lupunjaje ambae alimwakilisha Mkuu wa TAKUKURU wa mkoa wa Geita katika mkutano huo, akielezea wakati wa salamu zake jinsi waandishi wa habari walivyo wadau muhimu katika mapambano ya kukabiliana na Rushwa hapa nchini na kutoa Rai kwa wanachama wa Geita Press Club waendelee kuzingatia miiko na maadili ya uandishi ili sifa yao isichafuke kwani TAKUKURU inawategemea kuibua maovu katika jamii.

Pia amesema watu wachukue juhudi za makusudi kuwalinda watoto nyakati hizi za sikukuu na wasiachwe watembee wenyewe kwani kunaweza kusababisha wengine kupoteana na wazazi wao.

Kuhusu madereva wa vyombo vya moto, wakiwemo magari ya abiria, magari binafsi, bajaj na bodaboda kutojihusisha na unywaji wa pombe huku wakiwa wamebeba abiria na pia kuwa makini wawapo barabarani kwani wasafiri ni wengi hivyo wajiepushe na ulevi.

Katibu Mkuu Mtendaji wa klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Geita (Geita Press Club-GPC) Bw Novatus Lyaruu akifafanua jambo kwenye mkutano huo huku akiwa ameshikilia Katiba ya Geita Press Club-GPC wakati wa mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Bwalo la Jeshi la Polishi mjini Geita leo December 22, 2022.

Nae Kamanda wa TAKUKURU kutoka wilaya ya Geita ambae katika mkutano huo alimwakilisha Kamanda wa TAKUKURU wa mkoa wa Geita Bw Said Lipunjaje amewaeleza wanachama wa klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Geita yaani Geita Press Club kwamba, 

"Waandishi ni wadau wakubwa na tegemezi katika mapambano dhidi ya  Rushwa hapa mkoani Geita na pia kwa Taifa zima la Tanzania hivyo muendelee kufanya kazi zenu kwa weledi na kwa kuzingatia miiko na maadili ya uandishi wa habari bila kuyumbishwa" alisisitiza Afisa huyo.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Wilson Shimo (katikati mwenye kaunda suti ya bluu) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Geita (Geita Press Club) Bw Renatus Masuguliko (mwenye shati jeupe) kushoto kwa Mkuu wa Wilaya, pamoja na viongozi wengine na baadhi ya wanachama wa GPC mbele ya ukumbi wa Bwalo la Jeshi la Polisi la Mkoa wa Geita mara baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu Maalum wa GPC mjini Geita leo December 22, 2022.

Awali Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Geita (Geita Press Club) Bw Renatus Masuguliko aliuambia mkutano huo kwamba, ni mkutano mkuu maalum ambao lengo lake ni kupitia na kuidhinisha maazimio ya mkutano mkuu wa viongozi wa klabu zote za waandishi wa habari uliofanyika jijini Dodoma hivi karibuni chini ya usimamizi wa UTPC na kusema kwamba klabu hizo zimedhamiria kusonga mbele kwa kubuni miradi itakayo wasaidia kuwaletea kipato na hivyo kuimarisha utendaji wao wa kazi wa kila siku.

Mkutano huo ulipitisha pia maazimio yake binafsi ya utekelezaji, ambapo mwakani mwezi February 2023 utafanyika mkutano mkuu mwingine wa kawaida kulingana na katiba ya GPC.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments