Mwenyekiti wa jumuiya ya CCM wilayani Sengerema mkoani mwanza Jackson Mazinzi akikabidhi kadi na mihuli kwa baadhi ya viongozi kata Nyatukala |
Na Anna Ruhasha, Mwanza.
Jumla ya matawi ya Jumuiya ya wazazi CCM 197 wilayani sengerema mkoani Mwanza yameondokana na ukosefu wa mihuli na kadi za jumuiya hiyo baada ya Mwenyekiti wa wilaya Jacksoni Mazinzi kuchonga mihuli na kununua kadi zaidi ya 2000 na kuigawa bure kwa kila tawi kwa lengo la kuondoa changamoto hiyo iliyodumu kwa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi na viongozi walio pita.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara yake na kamati ya utekelezaji amesema mihuli na kadi za jumuiya ni sehemu ya ahaadi yake kwa wajumbe ambapo walimtaka akishika kijiti cha uongozi awatatulie changamoto hizo.
“Wakati nagombea mlinitaka nitatue changamoto za kadi na mihuli na mimi nimefanya hivyo mnakumbuka niliahidi kadi elfu moja lakini kulingana uhitaji nitatoa kadi bure 2250 kwa kata zote 47 za wilaya ya Sengerema niliahiadi natekeleza”alisema.
Kwa upande wake katibu wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Sengerema Jamali Athuman alitumia ziara hiyo kuwakumbusha wajumbe na wananchama wa jumuiya hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano na viongozi waliopo madarakani na kuendelea kusemea mazuri yanayofanywa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hususani ujenzi wa vyumba vya madarasa unaoendelea katika wilaya hiyo.
Hata hivyo baadhi ya viongozi kamati tekelezaji waliongozana na Mwenyekiti Dickson Mtaka na Josephat Makoli…walishauri kuwa ziara hiyo isiishie katika jumuiya ya wazazi badala yake kila jumuiya iwafikie wanachama na viongozi ili kuwasikiliza na kutatua kero zao kuliko kusubiri wakati wa uchaguzi.
Mwisho
0 Comments