TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

SERIKALI ITENDELEA KUWASAIDIA VIJANA WENYE MAWAZO CHANYA.

Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi Jenifa Omolo akimpongeza mwanafunzi bora wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) tawi la Mwanza Ndg Ally Sharif Shabaan wakati wa mahafali ya 36 ya chuo hicho duru ya pili Dicember 16, 2022 jijini Mwanza. Wengine wanao shuhudia ni Mkuu wa chuo hicho Prof Hozen Mayaya (kulia) na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa chuo, Prof Martha Qorro (kushoto)

Na Urban Epimark, MWANZA

Serikali imewahakikishia wahitimu wa Chuo cha Mipango na Maendekeo Vijijini (IRDP) kwamba itaendelea kuwatumia na kuwasaidia vijana wote watakao kuwa na mawazo chanya ili waweze kujiajiri na kuondoa umaskini katika jamii.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi Jenifa Omolo mwishoni mwa juma jijini Mwanza alipokuwa akiwatunuku vyeti vya kuhitimu masomo katika ngazi mbalimbali wahitimu 2691 wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP), tawi la Mwanza.

"Naomba muwe na moyo wa kuthubutu kufanyia kazi maoni yenu mlioyo yafanyia utafiti na katu msiogopeshwe na watu  wachache ambao walikuwa na mawazo kama yenu lakini wakashindwa. Serikali muda wote iko tayari kusaidia vijana wenye mawazo chanya ya kibiashara kutimiza malengo yao" alisema Naibu Katibu Mkuu.

Halikadhalika amewataka waadhiri wa chuo hicho kuendelea kuwasaidia wanafunzi katika chuo hicho kufanya tafiti zilizo mahiri na kuibua majibu ya changamoto zinazo wakabili vijana baada ya kuhitimu masomo yao na pia kusaidia kuwatafutia fursa za kupata mitaji ya kuendeleza mawazo yao waliyo yawasilisha katika tafiti zao.

Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi Jenifa Omolo (katikati johoo jekundu) katika mahafali ya 36 ya Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) duru ya pili akiwa na Mkuu wa Chuo hicho Prof Hozen Mayaya (kushoto kwake) na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa chuo hicho Prof Martha Qorro (kulia kwake) wakifurahia jambo wakati mahafali hayo yakiendelea katika viwanja vya chuo hicho jijini Mwanza Dicember 16, 2022

Nae Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa chuo hicho Prof Martha Qorro ameipongeza serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kujali na kuboresha zaidi mazingira ya utoaji elimu nchini ikiwemo kuondoa ada za masomo kuanzia ngazi ya awali hadi kidato cha Sita lakini pia kuongeza bajeti ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

"Kitendo cha ujenzi wa shule 26 za sayansi kwa ajili ya watoto wa kike, ujenzi wa shule mpya 234 za kata nchi nzima kwa kata ambazo hazikuwa nazo na shule nyingine 20  kwa ajili ya kupunguza msongamano na kuleta uwiano katika mikoa, ni moyo wa kijasiri alio nao Rais wetu Dkt Samia" aliongeza hivyo.

Akitoa shukrani kwa niaba ya menejimenti ya chuo Mkuu wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini Prof Hozen Mayaya alitoa shukrani kwa uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango  kwa kukiwezesha chuo hicho kupata bajeti ya kutosha ya ujenzi wa miundombinu ikiwemo madarasa, na kuwezesha kituo cha Mwanza kutoa wahitimu hao 2691 kwa mwaka huu.

Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi Jenifa Omolo (katikati johoo jekundu) akiwa katika maandamano ya kitaaluma ya Baraza la Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) wakati wa kuelekea kwenye eneo la mahafali ya 36 ya chuo hicho duru ya pili jijini Mwanza Dicember 16, 2022. Wengine katika mstari wa mbele ni Mkuu wa chuo hicho Prof Hozen Mayaya (kulia) na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa chuo hicho Prof Martha Qorro (kushoto) nyuma ya mbeba siwa.

Prof Mayaya aliendelea kusema kwamba, katika kuunga mkono juhudi za serikali kwenye masuala ya elimu, chuo kitaendelea kujizatiti kuandaa waalamu bora wenye weledi wa kutosha  katika fani za mipango ya maendeleo Vijijini na pia kutoa huduma iliyo bora kwa wadau wote.

Katika mahafali hayo ya 36 ya Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini duru ya pili, ambapo kwa kituo cha mafunzo cha Kanda ya Ziwa Mwanza kimeadhimisha mahafali hayo kwa mara ya kumi sasa na mwanafunzi wa ngazi ya Diploma Bw Ally Sharif Shabaan aliibuka mwanafunzi bora kwa kupata GPA ya 5.0 na kujizolea jumla ya Tuzo tano tofauti ya chuo hicho.

Tuzo hizo ni pamoja na Tuzo ya ufaulu wa kiwango cha juu, tuzo ya ufaulu mzuri zaidi ngazi ya Diploma na Tuzo ya Rais wa Convocation ya mwaka 2021/22.

Halikadhalika Tuzo nyingine ni ile ya Askofu Chiwanga inayo tolewa kwa mwanafunzi bora  kila mwaka na pia Tuzo ya Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini, ambayo ni ya hadhi ya juu kuliko zote.

Sehemu ya wahitimu na waadhiri wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) tawi la Mwanza wakiwa mbele ya meza ya Mgeni Rasmi wakati wa mahafali ya 36 ya chuo hicho duru ya pili jijini Mwanza Dicember 16, 2022. Jumla ya wahitimu 2691 walitunukiwa shahada mbalimbali na Mgeni Rasmi ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi Jenifa Omolo.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments