Na Alphonce Kabilondo ,Geita
SHIRIKA la kutetea haki za watoto, plan International limetoa msaada wa baiskeli miatano 500 kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi wakike wanaotembea umbali mrefu kwenda .
Mkurugenzi wa mradi wa kuwawezesha wanafunzi wa wakike wenye rika balehe kuendelea na masomo KAGIS Nicodemas Gachu amesema kuwa mradi huo unaotekelezwa kwa ufadhili wa serikali ya watu wa Canada kwa kushirikiana na Shirika la plan International kwa kipindi cha miaka mitano .
Alisema kuwa kati ya baiskeli hizo 300 zitagawanywa kwa wanafunzi wakike wanaotembea umbali mrefu kwenda shule katika Mkoa wa Geita na 200 kwa wanafunzi wa Mkoa wa Kigoma wanaotembea umbali mrefu.
Katika picha alievalia shati la drafti akitabasamu baada ya Mkuu wa wilaya Geita kukata utepe ni Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la Plan International Bw Peter Mwakabwale . |
Mradi huu utawawezesha wanafunzi wakike wenye rika balehe kuendelea na masomo na kuwa epusha na vishawishi vya kufanya mapenzi katika umri mdogo na kusababisha mimba za utotoni ''alisema Mkurugenzi huyo .
Mkurugenzi wa miradi ya shirika la plan International Nchini Peter Mwakabwale alisema kuwa shirika la plan limekuwa likifanya kazi mkoani Geita toka mwaka 2000. na kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya Elimu, kuzuia ajira hatarishi kwa Watoto, Usafi wa mazingira pamoja na ulinzi kupitia ufadhili wa Serikali ya Watu wa Canada (GAC) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania,
"Shirika la Plan International linaunga mkono juhudi za serikali, chini ya mradi huu wa KAGIS ambapo baiskeli 2,000 zitanunuliwa na kusambazwa kwa wanafunzi wa kike mpaka kukamilika kwa mradi huo pia mbali na mradi huo shirika hilo limekuwa likitekeleza miradi mbalimbali ikiwemo Elimu ,kuzuia ajira hatarishi kwa Watoto ,Usafi wa mazingira "alisema Mkurugenzi huyo .
Baadhi ya Wazazi na Wanafunzi waliohudhuria hafla ya ugawaji baiskeli kwa watoto wa kike Geita. |
Awali Mkuu wa Wilaya ya Geita Wilison Shimo aliyekuwa amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita kwenye hafla hiyo alliipongeza shirika na serikali ya watu wa Canada kwa wa mradi huo huku akisisitiza baiskeli hizo zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa badala ya kugeuka kuwa mali ya wazazi wa wanafunzi hao .
Baadhi ya Wanafunzi waliokabidhiwa baiskeli kama wanavyoonekana katika picha hii wakiwa na nyuso za furaha. |
Mwanafunzi wa shule ya sekondari Bung'wangoko Mkoani Geita Aneth Komanya akatumia fursa hiyo kulishukuru shirika hilo kwa msaada huo na kuahidi kusoma kwa bidii na kufikia malengo yao huku mwanafunzi Keflini wa shule ya sekondari Ihanamilo akisema kuwa awali walikuwa wakitembea umbali mrefu kwenda shule hivyo baiskeli hizo zitawasaidia kwenda shule na kufika kwa wakati na kuwaepusha na vishawishi njiani kutoka kwa mafataki .
MWISHO.
0 Comments