Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa GS1-TANZANIA Bi Fatuma Kange. |
Na Urban Epimark, DAR ES SALAAM
GS1-TANZANIA inakusudia kuzindua wimbo maalumu wa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuijenga vyema Sekta binafsi nchini ili ichangie vyema ukuaji wa uchumi kupitia mfumo wa kidigitali.
Akiongea jijini Dar es Salaam leo February 20, 2023 Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1-TANZANIA Bi Fatuma Kange amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameiongezea chachu zaidi na kuiimarisha sekta binafsi hususani kwa kuhimiza matumizi ya mifumo ya kidigitali katika ufanyaji biashara na kubadilishana taarifa za bidhaa na masoko kiulimwengu ambapo Tanzania ni mmojawapo.
Uzinduzi huo utafanyika siku ya Alhamisi February 23, 2023 kwenye Mkutano wa Chai wa GS1-TANZANIA (Breakfast meeting) utakao fanyika jijini Dar es Salaam ukumbi wa Kisenga LAPF, Kijitonyama na Mgeni Rasmi ni Mkuu wa mkoa Mhe. Amos Makalla.
GS1-TANZANIA ni taasisi ya sekta binafsi nchini inayo jishughulisha na usajili wa huduma za leseni za Barcodes pamoja na QR Code kwa bidhaa zinazo zalishwa na wenye viwanda hapa nchini pamoja na wajasiriamali wanao patiwa mikopo ya asilimia 10% kutoka kwenye mapato ya ndani ya Halmashauri zetu kote nchini.
Mwisho
0 Comments