Kamishna wa Fedha za Nje, katika Ofisi ya Rais inayo shughulika na Fedha na Mipango wa SMZ Bw Yusuf Ibrahim Yusuf akifunga mafunzo ya taarifa za Mfumo mpya wa ukusanyaji mapato leo February 23, 2023. |
Na Urban Epimark, ZANZIBAR.
Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) kimepongezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa kuanda na kuratibu vyema uandaaji wa Mfumo wa Ukusanyaji taarifa za mapato Zanzibar (ZAN-MUTM) kwa Halmashauri 11 za Serkali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
Pongezi hizo zimetolewa jijini Zanzibar leo February 21, 2023 na Kamishna wa Fedha za Nje, katika Ofisi ya Rais inayo shughulika Fedha na Mipango ya SMZ, Bw Yusuf Ibrahim Yusuf kwenye hafla ya kufunga mafunzo elekezi ya Matumizi ya Mfumo mpya na kupokea maboresho ya taarifa za ukusanyaji mapato.
"Napenda kutumia fursa hii kuwapongeza wataalam wetu kutoka Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) kwanza, kwa kufanya tafiti ya changamoto ya vyanzo vya mapato katika Halmashauri zetu, pili kwa usimamizi madhubuti tangu hatua ya awali ya uandaaji wa mfumo wenyewe" amesema Kamishna huyo.
Kamishna wa Fedha za Nje wa SMZ Bw Yusuf Ibrahim Yusuf akiongea na washiriki wa mafunzo ya mfumo mpya wa ukusanyaji mapato kwa Halmashauri 11 za SMZ, kwenye ufungaji mafunzo hayo jijini Zanzibar. |
Mafunzo hayo yaliyo washirikisha Maafisa Mapato, Maafisa TEHAMA na Makarani wa Mapato kutoka Halmashauri za SMZ, Bw Yusuf aliongeza kwa kusema kwamba Halmashauri za SMZ zimepangiwa malengo ya ukusanyaji mapato wastani unao zidi BIL 10/= kwa mwaka.
"Tulikuwa tunatafuta mbinu za kupata huo wastani au zaidi ya kiwango tulicho wekewa lakini tunapata changamoto lakini sasa kupitia mfumo huu mpya unao endelea kuandaliwa na nina uhakika tunaenda kufikia malengo" aliongeza kwa kusema hivyo.
Mhadhiri wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) Dkt Bonamax Mbasa akiongea kwenye hafla ya ufungaji mafunzo hayo jijini Zanzibar leo February 21, 2023 |
Kwa upande wa Chuo cha Mipango ambao ndio walio andaa mafunzo hayo, Mhadhiri Mwandamizi wa IRDP Dkt Bonamax Mbasa amesema mfumo huo unao endelea kuandaliwa na Jam Solutions Ltd ni matokeo ya utafiti wa changamoto za vyanzo vya mapato katika Halmashauri zetu za SMZ.
Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) kwa kushirikiana na Jam Solutions Ltd kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kuwezesha kuandaa Mfumo wa Ukusanyaji Taarifa za Mapato Zanzibar (ZAN-MUTM) ambapo kwa sasa zoezi hilo limefikia katika hatua ya kutoa Mafunzo Elekezi ya utumiaji wa mfumo huo, ambao utaleta manufaa makubwa zaidi.
Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Kamishna wa Fedha za Nje wa SMZ Bw Yusuf Ibrahim Yusuf (hayupo pichani) wakati akifunga mafunzo hayo leo jijini Zanzibsr |
Mwisho.
0 Comments