Kanisa Kuu Katoliki la Jimbo la Geita. |
Na Urban Epimark, GEITA.
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida, Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita Mhashamu Flavian Kassala ametangaza kufunga huduma zote za shughuliza za ibada katika kanisa kuu hilo la Jimbo la Geita kuanzia jana February 27, 2023 kufuatia uharibifu wa vifaa vya kanisa ulio tokea kanisani hapo.
Taarifa iliyotolewa leo February 28, 2023 mjini Geita na Kaimu Kiranja Mkuu wa Mapadre wa Jimbo hilo (Acting Vicar General) Padre Gerald Singu kwenda kwenye parokia zote imesema, ni kutoa nafasi ya mafungo maalum kumlilia Mungu kuhusu tukio hilo baya la kufuru na unajisi kwa kanisa.
"Wapendwa mapadre, kwa masikitiko makubwa naomba kuwatangazieni na kuwaomba muwatangazie waumini kuwa Kanisa Kuu la Jimbo (Geita) limefungwa kwa shughuli zote za maadhimisho kuanzia Jumatatu February 27, 2023.
Jimbo limeingia katika kipindi cha toba na malipizi kwa kufuru na unajisi iliofanyika kwa Ekaristi Takatifu na Utakatifu wa kanisa letu. Ibada hizi za toba ya malipizi zina muhusu kila muumini wa Jimbo letu la Geita" taarifa hiyo ilisema.
Sehemu ya vifaa vya kanisa vya kufanyia Ibada vilivyo haribiwa. |
Juzi usiku February 26, 2023 mtu mmoja alivunja mlango wa kanisa hilo na kuingia ndani na kuharibu vifaa vya kufanyia ibada pamoja na Msalaba Mkubwa ulio kuwepo mbele ya Altare kuu na kisha kuharibu mfumo wa kurekedia matukio ili kuzibiti usalama wa CCTV ulio kuwa umefungwa katika jengo la kanisani hilo.
Baada ya tukio hilo kuripotiwa rasmi polisi na kwenye vyombo vya habari na Askofu wa Jimbo hilo Mhashamu Flavian Kassala hapo jana, jeshi la polisi lilikuja na taarifa ya uchunguzi na kusema mhalifu aliye fanya hivyo alikuwa Mlevu wa pombe aliyekuwa amepindukia.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita ACP Safia Jongo amesema, aliyefanya uharibifu huo alikuwa Mlevi wa pombe. |
Taarifa hiyo ya polisi ilizidisha "sintofahamu" kwa wengi wa waamini na wakazi wa mji wa Geita kwa kujiuliza ni kwa vipi mlevi alewe kisha kwenda kufanya vitendo kama hivi kwenye nyumba ya ibada, jambo ambalo ni nadra sana kutokea.
Mwisho.
0 Comments