Na Urban Epimark, DAR ES SALAAM.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makala(CPA Tanzania) atafungua Mkutano wa Chai (Breakfast meeting) ulio andaliwa na GS1-TANZANIA, taasisi ya Sekta Binafsi inayo sajili leseni za Barcodes kwa bidhaa za wenye viwanda nchini Tanzania.
Mkutano huo unaofanyika asubuhi hii February 23, 2023 katika ukumbi wa Kisenga Hall, LAPF Kijitonyama mkoani DSM, unahudhuriwa na wanachama na wadau wa GS1-TANZANIA wanaozidi 600 na umefadhiliwa na Benki ya CRDB, Bank ya Mwanga Hakika Bank, UTT Hamis, BRELA, DRAFCO GROUP LTD, Agri-Coffee na wengine wengi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Mhe. Dkt Zainabu Chaula ni Mgeni Maalum mwalikwa na anategemewa kuzindua tukio la shughuli za utengenezaji BATIKI kwa Mjasiriamali kutoka mkoani Morogoro na pia kuzindua wimbo maalum wa kumpongeza Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuijali Sekta Binafsi nchini.
Muonekano wa ukumbi wa mkutano wa GS1-TANZANIA Breakfast Meeting unavyo onekana mbele. |
Wakati huo huo, Mrajisi na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini Dkt Benson Ndiege ameishukuru GS1-TANZANIA kwa jitihada zake kubwa za kuendeleza Sekta Binafsi nchini.
Mrajisi huyo amweleza hayo Mwenyekiti wa Bodi ya GS1-TANZANIA na wajumbe wake Ndg Jumbe Menye leo asubuhi katika ukumbi wa Kisenga Hall, LAPF Kijitonyama muda mfupi kabla ya kuanza mkutano wa GS1-TANZANIA Breakfast meeting.
Mwisho.
0 Comments