TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

KANYASU AJITOSA TENA UBUNGE GEITA MJINI, ASEMA HANA WASIWASI NA MCHUJO WA CCM

Na Theresia C Method,


Kanyasu akichukua fomu ya ubunge ofisi ya Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Geita

Geita, Juni 30, 2025 – Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini anayemaliza muda wake, Mheshimiwa Constantine John Kanyasu, ameonyesha nia ya kuendelea kulitumikia jimbo hilo kwa kuchukua rasmi fomu ya kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa muhula mwingine.

Kanyasu amepokea fomu hiyo leo katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Geita kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya, Michael Msuya, akieleza kuwa ana imani kubwa na mchakato mzima wa ndani ya chama.

Akizungumza mara baada ya kukamilisha hatua hiyo muhimu, Kanyasu amesema; “Katiba inaruhusu kupiga kura na kupigiwa kura, hivyo kujitokeza kwa wingi kwenye kugombea ni ishara nzuri ya chama kuwa hai”

Aidha, Kanyasu ameahidi kuendeleza kazi aliyoianza ya kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali ndani ya Jimbo la Geita Mjini ikiwa atapata ridhaa ya chama na wananchi kuendelea kuwakilisha bungeni.

Kwa sasa, mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu za kugombea nafasi ya ubunge ndani ya CCM unaendelea huku wanachama mbalimbali wakiendelea kujitokeza kuwania nafasi hiyo katika maeneo tofauti ya nchi.


Post a Comment

0 Comments