Na Urban Epimark, DAR ES SALAAM.
Serikali imeitaka jamaii ya watanzania kutumia vizuri fursa za biashara zinazo tolewa na serikali katika kuleta maendekeo ya jamii nchini na kusaidia kuondoa tatizo la ajira.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Mhe.Dkt Zainabu Chaula amewaambia washiriki wa Mkutano wa Chai (GS1-TANZANIA Breakfast meeting) ulifanyika leo February 23, 2023 jijini Dar es Salaam ambapo wenye viwanda na wajasiriamali zaidi ya 600 wanachama wa GS1-TANZANIA walishiriki.
"Mwaka jana January 2022 Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliunda rasmi Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa lengo la kuisaidia Jamii iweze kupata maendeleo kwa haraka kwa kurasimisha shughuli zao kuwa rasmi ili zitambulike serikalini na pia kutenga mfuko wa mikopo kwa wanawake usio kuwa na riba ili muweze kujiajiri, jamii itumie fursa hii vizuri acheni kulalamika" amesema Katibu Mkuu.
Pia ameipongeza taasisi ya GS1-TANZANIA kwa kazi kubwa na muhimu inayo fanya kusaidia kukuza sekta binafsi nchini na kuitaka jamii ijifunze kwa undani zaidi kazi zinazo fanywa na GS1-TANZANIA kwani wengi hawazielewi ikiwa ni pamoja na umuhimu wake katika matumizi ya bidhaa zinazo enda sokoni na kushauri wapate muda wa kujifunza zaidi faida za Barcodes kwenye bidhaa.
Ametoa mfano wa Taifa la Japan kwamba, hakuna bidhaa yeyote inayo ingia sokoni kutoka kwa mzalishaji bila kuwa na Barcodes kwani itakuwa nje ya mfumo na hivyo kuikosesha serikali mapato na kufifisha maendeleo ya jamii.
Baadhi ya wanachama wa GS1-TANZANIA wakiwa kwenye mkutano wa GS1-TANZANIA Breakfast meeting uliofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na zaidi ya washiriki 600 leo February 23, 2023. |
Mkutano huo ulihudhuriwa na takribani wawakilishi wa taasisi zote za umma zinazo husika na mpango wa urasimishaji biashara nchini pamoja na benki za CRDB na Mwanga Hakika Bank.
GS1-TANZANIA ilitumia mkutano huo kutambulisha huduma zake mpya za kufanya usajili na kupata leseni za Barcode kwa njia ya mtandao, mfumo mpya wa utambuzi wa taarifa za bidhaa unao tumika kiulimwengu kwenye mataifa makubwa na pia dhamira ya GS1-TANZANIA kuanza kuhudumia Sekta ya Afya hapa nchini.
Kwa upande wa serikali za mitaa yaani Halmashauri, uliwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi ambae aliambatana na Afisa Maendeleo ya Jamii pamoja na idadi ya wajasiriamali walio kopeshwa mikopo ya asilimia 10, kutoka kwa vikundi mbalimbali vya wajasiriamali.
Pia ulikuwepo uwakilishi wa kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) pamoja na baadhi ya wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka upande wa Tanzania Visiwani.
Mwisho.
0 Comments