Na Mwandishi wetu, Geita.
WAFANYAKAZI zaidi ya 40 wamepoteza ajira kutokana na miundombinu ya kuchakata dhahabu iliyopo katika Kijiji cha Ililika wilaya na Mkoani Geita kusimamishwa na Ofisi ya Madini Mkoa wa Geita kutokana na kudaiwa kuibuka mgogoro kati ya waliokuwa wabia wanaodai kuchangia kujenga miundombinu katika mgodi huo wa uchakataji madini.
Akithibitisha hivi karibuni kuwepo kwa hatua hiyo mwekezaji mzawa wa Leseni hiyo Elias Lukasi Kivuyo anadai kutoshirikishwa na baadhi ya maamzi yanayokinzana na uhalisia yanayotolewa na ofsisi ya madini mkoa wa Geita kumekuwa kunachangia kuibuka kwa baadhi ya migogoro, hatua ambayo wafanyakazi wa kutwa yaani vibarua 40 watapoteza fursa za kufanya kibarua,kumuathiri yeye mwenyewe kiuendeshaji pamoja na kodi za Serikali.
Kivuyo anadai kuwa kabla ya ofisi ya madini mkoa wa Geita kuchukua hatua iliyochukuliwa kulikuwepo na ubishani kuhusu badhi ya miundombinu waliyojenga pamoja na aliyekuwa mbia wake Richard Kasubi baada ya mkataba kati yao wa kufanya kazi uliomalizika mwaka jana 2022, na hivyo kuhitaji majadiliano au tafasiri ya kisheria hatua mabayo imefanywa na ofisi ya madini Mkoa kama kumshinikiza ili akubali hatua anayoipinga akidai kuna dalili za uonevu.
Mabishano hayo yalihusu miundombinu iliyojengwa kwa ubia wakati wakiwa wabia kufanyiakazi ndani ya Leseni ya Uchimbaji ya Elias Lukasi Kivuyo baada ya kupata leseni ya ubia ya uchakataji madini kwa kufanyia katika eneo la Elias Lukasi Kivuyo na aliyekuwa mbia wake Kasubi ibakie kuwa mali ya nani baada ya mkataba kutokana na mkataba husika kutosema chochote juu ya kipengele hicho mara baada ya mkataba kumalizka.
Kivuyo anadai kuwa alimkaribisha aliyekuwa mbia wake Richard Kasubi kuingia nae ubia kufanya kazi katika leseni yake ya uchimbaji katika kitalu chake kilichopo katika kitongoji cha Ililika ambapo kupitia leseni ya ubia wao ya kuchakata madini Processing License No:0006 wakiwa wabia.
Aidha kwa ajili ya kuchakata dhahabu eneo la Ililika katika kata ya Nyarugusu wilayani Geita na Richard Kasubi aliamua kufungua shauri la madai katika mahakama ya mwanzo Busanda /Nyarugusu mwaka jana 2022 akidai ni madai yanayotokana na kuwekeza katika ubia wao baada ya mkataba wao kumalizika.
Hata hivyo baada ya kuanza kulisikiliza shauri hilo mahakama hiyo ilibaini kuwa haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kutokana na kiwango cha shilingi milioni 75 kilichokuwa kimefunguliwa kwa mdai kuwa mahakama ya mwanzo haikuwa na mamlaka ya kulisikiliza na hivyo kulifuta kwa kumuelekeza mdai Richard Kasubi akafungue shauri hilo katika mahakama ya wilaya hatua ambayo haikutekelezwa na mdai kwa wakati huo.
Kutokana na kutokea kwa mazingira hayo mmiliki wa kitalu kulipokuwa kunafanyika uchakataji kwa ubia Elias Lukasi Kivuyo anadai nae aliwasilisha katika mahakama hiyo ya Mwanzo ya Busanda /Nyarugusu madai dhidi ya aliyekuwa mbia wake Richard Kasubi kuendelea kufunga moja ya chumba ambacho kilidaiwa kuhitajika kutumika kwa ajili ya shughuli zingine za mgodi kilichokuwa kinatumika kwa ubia kabla ya mkataba kumalizika.
Kufuatia hatua hiyo Mahakama ya mwanzo Busanda /Nyarugusu Oktoba 30 mwaka 2022 ilitoa agizo kwa mwenyekiti wa kitongoji cha Ililika katika kata ya Nyarugusu ilipo leseni na miundombinu ya kuchakatia dhahabau inayobishaniwa asimamie utekelezaji wa kufungua chumba husika na kisha Mahakama iairifiwe kuhusu Utekelezaji huo.
Hata hivyo baada ya utekelezwaji huo Richard Kasubi aliyekuwa mbia wa Elias Lukasi Kivuyo alianza kulalamikia hatua hiyo akidai chumba kilichovunjwa alikuwa amehifadhia kaboni zake kutokana na kuvunjwa kufuli na kuwekwa kufuli jingine wakati yeye akiwa hayupo madai yanayopingwa na Elias Lukasi Kivuyo kuwa hatua hiyo ilikuwa ni utekelezwaji wa agizo la Mahakama iliyotolewa kwa mwenyekiti wa kitongoji cha Ililika Paulo Luhende na tayari mkataba ulikuwa umesha malizika wa ubia wao.
Akizungumzia madai hayo mwenyekiti wa kitongoji cha Ililika Paulo Luhende anakiri kutekeleza agizo hilo ikiwa ni amri halali ya mahakama ya mwanzo Busanda/Nyarugusu ililyotolewa Oktoba 30 mwaka jana 2022 na kuwa baada ya kuitekeleza alirejesha taarifa ya utekelezaji huo kwa mahakama kuhusu Utekelezaji huo uliofanyika hadharani.
Hata hivyo kwa upande wake yeye kama aliyekuwa amepokea jukumu la kutekeleza amri hiyo ya mahakama anasema wakati wa kutekeleza jukumu hilo walikuta hakuna kitu chochote cha thamani ndani ya chumba hicho isipokuwa malapa lapa ya mifuko ya sandarusi na uchafu unaotokana na chumba hicho kufungwa kwa muda mrefu na hapakuwepo na kaboni kama inavyodaiwa.
Awali akiuzngumzia madai hayo Richard Kasubi alisema kuwa alikuwa ameingia katika mgogoro na aliyekuwa mbia wake Elias Lukasi Kivuyo ambaye waliingia nae Ubia ili kufanya kazi pamoja ambapo walijenga baadhi ya miundombinu kwa pamoja na ili kufanikisha uendeshaji lakini katika eneo la Elias Lukasi Kivuyo na kupata Leseni ya uchakataji namba 0006 M/S Richard Kasubi &Lukasi Ole Kivuyo Oktoba 16 mwaka 2012 kila mmoja akiwa na hisa ya asilimia 50.
Kasubi aliongeza kudai kuwa tatizo lilianza baada ya mkataba kukoma wa ubia wao wa leseni ya kuchakata madini namba PCL 0006 mkataba wao haukuwa umesema lolote mara baada ya mkataba wao kukoma wa ubia miundombinu itakuwaje hatua ambayo imeibua sintofahamu hivyo kuhitaji majadiliano au tafasiri ya kisheria na vyombo vya kutoa haki.
Aidha katika hatua nyingine Richard Kasubi anadai kuwa kuvunjwa kwa chumba anachodai alikuwa amehifadhia kaboni zake hatua anayodai hakubaliani nayo ya kuvunjwa chumba bila yeye kuwepo hatua inayozidi kuongeza mvutano zaidi kati yao wakati Elias Kivuyo na Mwenyekiti wa kitongoji cha Ililika Pualo Luhende wakikanusha madai ya Richard Kasubi kuwa hayana ukweli na kuwa utekelezaji huo ulifanyika kwa agizo halali la Mahakama ya mwanzo Busanda/Nyarugusu.
Kaimu Afisa madini Mkazi mkoa wa Geita Martine Shija amekiri kuwepo kwa hatua hiyo na mgogoro huo lakini atalitolea ufafanuzi baada ya kupata kibali cha kuzuangumza na wanahabari atakapokuwa amepta kibali kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini.
0 Comments