TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

WANAFUNZI WAJENGEWE UJASIRI WAKUFICHUA UKATILI NA UNYANYASAJI KIJINSIA

Robert Nyamaigoro Mwenyekiti waJumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi  CCM wilaya ya Geita  wakati akizindua  utekelezaji  wa mwongozo  wa utoaji  Uji na Chakula  kwa wanafunzi  shuleni  

Na  Renatus Masuguliko, Geita.

WALIMU na wazazi wametakiwa kushirikiana na walimu kuwajengea ujasiri  wanafunzi  kuvifichua vitendo  vya ukatili  na unyanyasaji wakijinsia  wanaotendewa   wawapo shuleni na majumbnni  ili kujenga jamii yenye amani na ustaarabu.

Robert Nyamaigoro Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi  CCM wilaya ya Geita  akiwamiminia uji Wanafunzi. 

Wito huo umetolew ana  Robert Nyamaigoro Mwenyekiti waJumuiya ya Wazazi ya Chama cha mapinduzi wilaya ya Geita  wakati akizindua  utekelezaji  wa mwongozo  wa utoaji  Uji na Chakula  kwa wanafunzi  shuleni  kiwilaya   uliofanyika katika shule ya Msingi  Mbugani  iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Geita yenye wanafunzi zaidi ya 2,220.

Robert Nyamaigoro Mwenyekiti waJumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi  CCM wilaya ya Geita  akimtaka mwanafunzi alete kikombe awekewe uji wakati wa uzinduzi wa programu ya uji mashuleni Wilaya ya Geita 

Rehema Mtawala ni Katibu wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Geita  na Emmanuel Fortunatus ni Mqwewnyekiti wa CCM kata ya Kalangalala  waliomo kwenye kamati  kazi ya kuhakikisha  zoezi hilo linafanikiwa. 

 Ramadhani  Lukasi Mkome ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Geita akashiriki katika uzinduzi  huo kwa vitendo  kwa kuchangia   huku mwnyekiti wa mtaa wa Mbugani John Joachim wanabainisha   walivyojipanga  kusimamia mpango huo. 

Robert Nyamaigoro Mwenyekiti waJumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi  CCM wilaya ya Geita akiwa na viongozi wenzake katika Shule mojawapo Wilaya ya Geita 

Awali Mwalimu mkuuw a Shule hiyo  ya Mbugani Edwick Ndunguru  pamoja na kudai kuwepo kwa baadhi ya changamoto  lakini akatumia fursa hiyo  kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa serkali yake kuipatia   shule hiyo zaidi ya shilingi milioni 330 kwa ajili ya  ujezni  wa miundombinu   ikiwemo  ujezniwa Bweni  kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

waJumuiya ya Wazazi ya Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Geita  wakati akizindua  utekelezaji  wa mwongozo  wa utoaji  Uji na Chakula  kwa wanafunzi  shuleni  


Mwisho

Post a Comment

0 Comments