TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

ATCL KUTOA PUNGUZO KWA SMEs WENYE BARCODES ZA GS1-TANZANIA KUPELEKA BIDHAA ZAO SOKO LA INDIA & ULAYA.



Urban Epimark, Dar es Salaam. 

Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limesema linaanda mpango mahususi wa kusaidia wajasiriamali wa Tanzania (SMEs) wenye bidhaa zenye Barcodes kutoka GS1-TANZANIA kusafirisha bidhaa zao kwa bei punguzo kwenda kuuza kwenye masoko ya India, Falme za Kiarabu na Ulaya.


Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi amewaambia washiriki wa Mkutano wa wadau wa usafirishaji mizigo kwa njia ya Anga kilichofanyika jijini Dar es Salaam March 20, 2023.

Katika mkutano huo ambao ulijadili kwa kina fursa za usafirishaji mizigo kwa njia ya Anga kilichoandaliwa na ATCL na kushirikisha wadau katika sekta hiyo nchini, Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1-TANZANIA Bi Fatuma Kange alichangia hoja kwamba, wakati umefika kwa ATCL na wadau wengine nchini kuunga mkono jitihada za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kuifungua nchi kiuchumi na kusaidia SMEs wa Tanzania kusafirisha bidhaa zao kwenda kuuza kwenye masoko ya nje ya nchi kwa gharama nafuu.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments