TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

BAADHI YA WATAALAMU KUTOKA CCBRT WATOA KONGOLE KWA FURAHA MATONDO MBUNGE

Neofitha Lukilingi mtaala wa viungo kwa watu wenye ulemavu akiongea na wananchi katika mkutano wa mbunge wa viti maalum Furaha Matondo akitoa elimu matumizi sahihi ya Viti mwendo. 

Na Anna Ruhasha, Mwanza. 

Mtaalamu wa walemavu wa viungo kutoka CCBRT amewataka wazazi na walezi kuhakikisha kila kifaa cha kumsaidia mlemavu wa viungo hususani miguu kama vile kiti Mwendo au baiskeli wanapimwa kabla ya kutumia vifaa hivyo ili kudhibiti madhara ambayo yanaweza kutokea kutumia kifaa kisichomtosha wakati amekaa. 

Kauli hiyo imekuja wakati Neofitha Lukilingi mtaalamu wa viungo kwa walemavu kutoka CCBRT akiwafanyia vipimo vya urefu na upana baadhi ya walemavu waliofikiwa na msaada wa viti mwendo kutoka kwa mbunge viti maalum mkoa wa Mwanza Furaha Matondo.

Amesema baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwanunulia au wakipewa kama alivyofanya Mbunge Furaha lakini hawatumii watalaamu kuhakiki kama kifaa hicho kinafaa au la, badala yake wanatumia na baadhi ya walemavu wanaokaa sana wanapinda migongo na wengine wanapata vidondo vikubwa ambapo amesema hiyo husababishwa na ukubwa au udogo wa kifaa na kusema kwamba ndio maana vinafanyika vipimo ili kuondoa changamoto hiyo.

Aidha, Lukilingi ameongeza kuwa tangu ameanza kufanya kazi kitengo cha viungo ni zaidi ya miaka kumi na moja lakini hajawai kuona kiongozi alietumia rasilimali zake kwa kutafuta viti vyenye gharama kila kiti mwendo kinanunuliwa shilingi mia saba elfu (Tsh. 700,000/=) na kutafuta wataalamu ili kuwafanyia vipimo walengwa kabla ya matumizi ni jambo kubwa ambalo amelifanya Mhe. Matondo kwenye jamii halitasahaulika ambapo amewaomba wananchi wa mkoa wa Mwanza kuendelea kumuunga mkono Mbunge huyo.

Baadhi ya wananchi wakizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa hadhara katika zoezi la kuwapati viti mwendo na fimbo kwa baadhi ya walemavu wa macho na miguu wamesema kuwa wabunge wengi wamekuwa hawawakumbuki watu wenye mahitaji maalumu badala yake wamekuwa wakitumia fedha zao kuwasaidi wajumbe walio wapigia kura ya kuwapitisha kugombea nafasi hizo pekee na kuwasahau wapiga kura wao ambao ni wananchi wakiwemo watu wenye mahitaji maalum. 

Hata hivyo akikabidhi viti mwendo na fimbo Mbunge Matondo amesema anaimani wale wanaonufaika na mikopo inayotolewa na halmashauri watafanya biashara zao wakiwa wamekaa kwenye viti na kutembea kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine bila bugudha.

Halikadhalika Mbunge Matondo ameitaka jamii kutoficha majumbani watoto wenye ulemavu badala yake wawapeleke shuleni ili waweze kutimiza ndoto zao kwa kupata Elimu. 

Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments