TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

BIMA YA AFYA YAJA NA MFUMO MPYA KWA WATOTO.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya Nchini (NHIF) Bw.Benard Konga.

Na Urban Epimark,  DODOMA

Mfuko wa Bima ya Afya nchini (NHIF) umetangaza mfumo mpya wa kuwasajili watoto chini ya miaka 18 kupata huduma za afya  kupitia shule wanazo soma badala ya ule wa zamani wa  kupitia "Toto Afya Kadi" 

Mfuko huo umewashauri wazazi na walezi kuwasajili watoto wao kama wategemezi wao kwenye bima ya afya au kuwasajili kupitia shule wanazosoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Bw. Benard Konga ameeleza hayo leo  Machi14, 2023  Jijini Dodoma wakati alipoongea na Waandishi wa Habari kuhusiana na maboresho katika utaratibu wa usajili wa watoto.

Konga amesema kuwa lengo la kufanya hivyo  ni kuongeza wigo wa wanachama katika mfumo wa Bima ya Afya kuelekea Bima ya Afya kwa wote na kuhakikisha wanachama katika makundi hayo wanajiunga kama familia au kaya  ya wanafunzi kupitia shule wanazosoma.

"Mpango wa Toto Afya Kadi ulianza rasmi  Mwaka 2016 baada ya kufanyiwa upembuzi na lengo ikiwa ni kuwajumuisha watoto kupitia shule zao" amesema. 

Aidha amebainisha kuwa  nia ni kufikia kundi kubwa la watoto walio chini ya umri wa miaka18 ambao kitakwimu  ni zaidi ya nusu ya wananchi wote ili kufikia azma ya serikali ya watu wote kuwa na bima ya afya kwani sensa ya 2022 inaonesha idadi ya watoto chini ya miaka 18 ni asilimia 31% ya wananchi wote.

Licha ya hayo, Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kuwa uzoefu wa miaka saba wa kulihudumia kundi hilo la watoto kupitia utaratibu wa Toto afya kadi umewezesha mfuko kufikia watoto 210,664 walio chini ya miaka18. 


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments