TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

BUCHOSA YAPITISHA BAJETI YA BILIONI 33.7, 2023/2024

Kaimu mkurungenzi halmashauri ya Buchosa Mwita Waryoba akiwasilisha mpango wa mapendekezo ya bajeti katika baraza la madiwani halmashauri ya Buchosa mkoani Mwanza.

Anna Ruhasha, Mwanza. 

Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imepanga kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi za Tanzania bilioni 33.7 kutoka vyanzo mbali mbali vya mapato ili kutekeleza shughuli za maendeleo.

Akiwasilisha mpago wa bajeti hiyo  Kaimu mkurungenzi wa halmashauri ya Buchosa  Mwita Waryoba  amesema kuwa Mapato ya ndani wamekadiria  kutumia bilioni 3.8 ikiwa ni pamoja na ruzuku ya mishahara, ruzuku ya matumizi mengineyo na ruzuku ya miradi ya maendeleo.

Baraza la madiwani baada ya kupitisha  bajeti hiyo Diwani wa kata ya Kazunzu Boniphace Msenyela na Diwani wa kata ya Bupandwa Masumbuko Bupamba  wakizungumza kwa niaba ya wenzao wameipongeza ofisi ya mkurungenzi  kwa kuaanda mpango wa bajeti  kwa kuainisha kila kata na kwa uwazi hali iliyosaidia kupunguza maswali katika kikao hicho.

Madiwani wa halmashauri ya Buchosa katika kikao cha mapendekezo ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Hata hivyo Mwenyekiti wa halmashauri ya Buchosa Mhe. Idama Kibanzi  amesema kuwa  tumaini la baraza hilo nikuona bajeti hiyo inarudi kama ilivyopendekezwa huku akimuomba Mbunge wa jimbo hilo Eric Shigongo pamoja na mkurungenzi kwenda kuitetea wawapo Bungeni wakati wa kikao cha Bajeti.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments