Askofu Mstaafu jimbo Katoliki Dar es Salaam Kadinali Pengo. |
Na Urban Epimark, Geita Tanzania.
Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Katoliki la DSM Polycarp Kadinali Pengo atawaongoza maaskofu wenzake kutoka Baraza La Maaskofu Katoliki Tanzania-TEC jumamosi ijayo March 18, 2023 mjini Geita kulitabaruku upya Kanisa Kuu Katoliki la Jimbo la Geita lililo najisiwa na mlevi mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.
Taarifa fupi iliyo tolewa mjini Geita leo asubuhi March 11, 2023 imesema yatafanyika maandamano ya maaskofu, mapadre na waamini wote kutoka Parokia jirani ya Bikira Maria wa Fatima ya mjini Geita kuelekea Kanisa Kuu na takribani maaskofu wote kutoka TEC na wageni wengine waalikwa watashiriki.
Kanisa hilo lilifungwa kwa shughuli za kichungaji na maadhimisho ya Misa Takatifu mnamo Februari 26 hadi kufikia hiyo March 18, 2023 baada ya Askofu wa Jimbo hilo Mhashamu Flavian Kassala kutoa waraka maalum wa kanisa kuingia kwenye mafungo ya kumlilia Mungu na kuomba Huruma yake kwa kufuru na unajisi uliofanywa kwa kanisa hilo na kijana mmoja ambae baadae ilithibitika kuwa ni mlevi.
Mwisho.
0 Comments