Mwenyekiti wa Kamati ya siasa wilaya akitoa agizo hilo wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua miradi inayotekelezwa kuanzia mwaka wa fedha 2022/2023. |
Na Anna Ruhasha, Mwanza.
Wananchi wametakiwa kushirikishwa kabla ya utekelezaji wa miradi katika maeneo yao ili kuondoa manung'uniko na maswali mengi pindi viongozi wa Chama cha Mapinduzi wanapofanya ziara ya ukaguzi katika miradi hiyo.
Agizo hilo limetolewa na kamati ya siasa wilayani Sengerema mkoani Mwanza wakati ilipofanya ziara katika miradi mbali mbali ya maendeleo katika halmashauri ya Buchosa mkoani hapa .
Mack Agustine Makoye (DM) mwenyekiti wa CCM wilaya ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya Siasa wilaya amesema kuwa lengo la kamati ya siasa kukagua miradi ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho kwa lengo la kujilidhisha fedha na thamani ya mradi na ushirikishwaji wa wananchi kama unazingatiwa wakati wa utekelezaji wa mradi husika.
Baadhi ya wajumbe katika mradi huo pamoja na Kaimu katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Sengerema Adamu Itambu. |
Aidha, DM pamoja na wajumbe wa kamati ya siasa na sekretariet katika ukaguzi wa bwawa la umwagiliaji katika kijiji cha Sukuma kata ya Bukokwa wameshauri wananchi kushirikishwa miradi kabla ya kutekelezwa ambapo hii itaondoa maswali kwa viongoz wakati waziara za ukaguzi wa miradi hiyo .
Mwenyekiti wa UWT wilaya Jenny Msoga memtaka mkandarasi kukamilisha mradi huo kwa wakati ili kusudio la wakazi wa Sukumu kunufaika na mradi huo unatimia ili waweze kufanya kilimo biashara.
Mhandisi Msimamizi wa Miradi ya Umwagiliaji Magurukenda-Sukumu akitoa maelezo juu ya ujenzi wa mradi huo ambapo amesema unatalajia kukamilika Septemba 27 2024. |
Baadhi ya wananchi walioshiriki katika ukaguzi wa mradi wa bwawa la umwagiliaji wameishukuru serikali na kusema kuwa kilimo cha umwagiliaji kitakuwa mkombozi na kuongeza kipato kwa mtu mmoja mmoja, jamii na serikali kwa ujumla.
Hata hivyo kilio cha vibarua wanao fanya kazi katika ujenzi wa mradi huo wamesema changamoto kubwa inayowakabili ni kucheleweshewa malipo na kuiomba kamati ya siasa kuingilia kati na kulipwa kwa mujibu wa mkataba unavyosema.
Akitoa taaarifa mbele ya kamati ya siasa na viongozi wa serikali ambao wamefanya ziara ya ukaguzi wa mradi huo, Mhandisi msimamizi miradi ya umwagiliaji Magurukenda na Sukuma Mwampulule Malichela amesema kuwa mradi huo utaghalimu Tsh.4,014,684,629.80.
Baadhi ya wataalamu na wananchi katika mradi wa bwawa la umwagiliaji kijiji cha Sukumu kata ya Bukokwa baada ya kamati ya siasa kufanya ukaguzi wa ujenzi wa mradi. |
Ameogeza kuwa kukamilika kwa umradi huo kutaongeza ajira kwa wananchi, kuwa na kilimo cha uhakika,kuongeza mapato ya halmashauri, uwepo wa maji ya uhakikia kwaajili ya mifugo hata matumizi ya kawaida na kuleta maendeleo ya kiuchimi na wakulima 1150 watanufaika na kilimo cha umwagiliaji.
Mwisho.
0 Comments