Baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa CCM wakikagua sehemu ya kuchoma takataka. |
Na Anna Ruhasha, Mwanza.
Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani Sengerema mkoani Mwanza imetembelea na kukagua kituo cha afya Kagunga ambapo wame pongeza uongozi wa kituo hicho kwa kutunza mazingira.
Mack Augustine Mwenyekiti wa kamati ya siasa ametoa pongezi hizo wakati walipotembelea kituo hicho na kukagua ujenzi wa nyumba za watumishi.
Aidha, kituoa hicho kinakabiliwa na changamoto ya maji hali inayo pelekea wagonjwa wanaopata huduma katika kituo hicho kuiomba serikali kutatua changamoto hiyo.
Katibu wa UWT na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Makoye akisalimia wagonjwa katika kituo cha Afya Kagunga pamoja na kukagua vifaa tiba. |
Hata hivyo, katibu wa UWT Sengerema katika ukaguzi wa kituo hicho amesisitiza kuongeza hali ya usafi wa vyoo vya akina mama wanao subiri kujifungua huku
akisikitishwa na vyoo hivyo kuwa nje ya wodi ya Wazazi ambapo vyoo vizuri na visafi vilivyoko ndani ambavyo wangetumia wamama hao vikitumiwa na watumishi wa hospitali hiyo.
Mwisho.
0 Comments