Mhe Furaha Matondo akizungumza katika mkutano wa hadhara wakati akikabidhi viti mwendo kwa watu wenye mahitaji maalumu wilayani sengerema mkoani Mwanza. |
Na Anna Ruhasha, Mwanza.
Mbunge viti maalum mkoa wa mwanza Furaha Matondo ameitaka jamii kuwalinda na kuwapenda na kuacha kuwanyanyapaa watu wenye ulemavu ambapo amesema watu hao ni watu kama watu wengine wanahaki ya kusaidiwa na kupewa vitendea kazi na mitaji pia.
Picha ya baadhi ya viti mwendo kutoka kwa Mhe Mbunge viti maalum mkoa wa Mwanza Bi. Furaha Matondo. |
Mbunge Matondo amesema hayo wakati wa zoezi la kutoa viti mwendo 16 wilayani Sengerema mkoani Mwanza kati ya viti hivyo, viti (8) nane vimetolewa kwa walemavu waishio halmashauri ya Buchosa na viti nane (8) vilivyo baki vimetolewa kwa walemavu wanaoishi katika halmashauri ya wilaya ya Sengerema.
Aidha, Mhe Matondo amesema anakila sababu ya kutoa viti mwendo hivyo maana vitawasaidi walemavu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa urahisi.
Baadhi ya wataalamu wa ulemavu wa viungo kutoka CCBRT wakionyesha jinsi ya matumizi sahihi ya viti mwendo hivyo baada ya kuwapima na kuhakikisha wanakaa bila bugudha. |
“Ndugu zangu wananchi na walemavu mlioko hapa kwa kuguswa na changamoto mnazozipitia hasa kutoka sehemu mmoja kwenda sehemu nyingine nimetoa viti mwendo 70 kwa baadhi ya walemavu kwa wilaya zote za mkoa wa Mwanza lakini pia na fimbo kwa ndugu zangu vipofu.”
Baadhi ya wazazi na walezi wa walemavu wa viungo vya miguu na macho wakipokea vifaa hivyo wamemshukuru mbunge huyo kwa kutumia sehemu ya mshahara wake kuwasaidi watu wenye uhitaji ambapo wameahidi kuvitunza katika mazingira mazuri.
Picha ya pamoja baadhi ya walemavu waliopokea kwa furaha viti mwendo kutoka kwa Mbunge viti maalum mkoa wa Mwanza. |
Nao baadhi ya watu wenye ulemavu licha ya kushukuru wameomba viongozi kuiga mfano kwa Mbunge Matondo ambaye amekuwa mfano boro kwa jamii kuwafikia watu wenye uhitaji zaidi.
Mwenyekiti wa UWT wilayani Sengerema Jenny Msoga ametumia nafasi hiyo kumshukuru mbunge Furaha Matondo kurudisha furaha kwa watu wenye mahitaji maalum ambapo amesema kuwa wataendelea kumpa ushirikiano wa kutosha kwani amekuwa kiongozi wa kusaidia jamii zenye uhitaji.
Baadhi ya wataalamu wa ulemavu wa viungo kutoka CCBRT wakionyesha jinsi ya matumizi sahihi ya viti mwendo hivyo baada ya kuwapima na kuhakikisha wanakaa bila bugudha. |
“Tunakushukuru Mbunge wetu ,tunawashukuru wataalamu kutoka CCBRT kukubali kuambatana na mama huyu mbunge kuja kutoa vipimo kwa ndugu zetu kabla hawajapewa viti mwendo hivyo unasifa ya mitano tena mbungeni" amesema Msoga.
Hata hivyo katika taarifa iliyosomwa na katibu wa UWT Sengerema Rosemary Mwakisalu amesema Mhe Furaha amekuwa msaada mkubwa wa kujitoa na kuchangia mambo mbali mbali kwenye jamii na kwenye chama ambapo pia amesha toa shuka kwa wagonjwa katika kituo cha afya Project , amechangia ujenzi wa mradi wa choo cha UWT na kununua mashine ya kudurufu (Photocopy machine) katika ofisi ya UWT Sengerema.
Picha ya pamoja baadhi ya walemavu waliopokea kwa furaha viti mwendo kutoka kwa Mbunge viti maalum mkoa wa Mwanza. |
Mwisho
0 Comments