TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

WANAWAKE WAJASIRIAMALI NGAZI ZA VIJIJI/KATA WASAIDIWE KUTANGAZA BIDHAA ZAO KIDIGITALI.

Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Taasisi inayo jishughulisha na kusajili mifumo ya Barcodes kwa wazalishaji bidhaa wa Tanzania kupitia GS1-TANZANIA Bi Fatuma Kange 

Na Urban Epimark, Dar es Salaam.

Serikali imeombwa kuandaa mpango mahususi na kutenga bajeti ya kusaidia utoaji elimu ya matumizi bora ya simu janja (smartphones) kwa wanawake wajasiriamali ngazi za vijiji na kata hapa nchini  ili kusaidia kutangaza na kupata masoko  ya bidhaa wanazo zalisha kupitia mitandao ya kijamii na kuchagiza kasi ya ukuaji uchumi kwenye sekta ya ujasiriamali na kuwaongezea kipato zaidi.

Ombi hilo limetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Taasisi inayo jishughulisha na kusajili mifumo ya Barcodes kwa wazalishaji bidhaa wa Tanzania kupitia  GS1-TANZANIA Bi Fatuma Kange mwishoni mwa juma  alipokuwa akihojiwa na Radio Deutsche Welle (DW) ya Ujermani kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Ulimwenguni mwaka huu na kauli mbiu yake "Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia ni Chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia"

"Mwanamke aliyeko Kigoma anae fanya biashara ya Migebuka au aliyeko Mtwara anae fanya biashara ya Korosho asaidiwe kutangaza biashara zake na kufikia wateja ulimwenguni kupitia smartphones yake baada ya kupatiwa elimu ya kuzitumia kwa faida zaidi" alisema Bi Fatuma Kange.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments