TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

JUWADA MUWE KIOO CHA MABADILIKO YA WANAWAKE KIUCHUMI: RC MAKALA

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makala akitoa hotuba yake wakati wa kufungua mafunzo ya viongozi wa JUWADA katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam Mei 03, 2023

Na Urban Epimark, Dar es Salaam.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makala amewataka viongozi wa Jukwaa la Wanawake Dar es Salaam (JUWADA) kuendelea kuwa kioo katika kuhuisha mabadiliko ya wanawake kiuchumi na kusaidia jamii itoke katika umaskini.

Pia amezitaka mamlaka za usimamizi na uzibiti katika mambo ya biashara zikiwemo TBS, TMDA, OSHA, TRA, SIDO na zingine kushirikiana kwa karibu zaidi katika kuwasaidia wanawake kujikwamua katika shughuli zao za kiuchumi na si kutumia sheria kuwakandamiza bali wawaelekeze njia ya kutatua changamoto zilizopo.

Mhe Makala aliyasema hayo kwenye hotuba yake ya ufunguzizi wa mafunzo maalum kwa viongozi wa JUWADA yaliyo andaliwa na Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) na kufadhiliwa na Benki ya CRDB na kufanyika kwenye Ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa JNICC jijini Dar es Salaam Mei 03, 2023.


Sehemu ya washiriki wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa viongozi wa JUWADA uliofanyika jijini Dar es Salaam Mei 03, 2023 akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi Rehema Madenge, wakuu wa wilaya za Kinondoni, Ilala, Temeke na Kigamboni pamoja na makatibu tawaka wao (ma-DAS) na viongozi wa majukwaa ya kiuchumi ya wanawake mkoani Dar es Salaam wakimsikiliza Mkuu wa mkoa Mhe Amos Makala wakati wa ufunguzi.

"Nawapongeza sana viongozi wa JUWADA mlio chaguliwa kuwaongoza wanawake wenzenu katika mkoa wa Dar es Salaam akiwemo Mwenyekiti wenu Bi Fatuma Kange ambae tuna mfahamu vizuri sana katika kuwasaidia wanawake wainuke kiuchumi. Endeleeni kuwa kioo cha matumaini na mafanikio kwa Mkoa wa Dar es Salaam" alifafanua Mhe Makala.

Wakati huo huo Mwanaharakati wa siku nyingi wa kutetea haki za kijinsia kwa wanawake Bi Gema Akilimali katika mafunzo hayo aliwasilisha mada ya Bajeti ya Kijinsia katika maendeleo ya jamii kupitia shughuli za kiuchumi zinazo fanywa na wanawake na kuwata wajenga tabia ya kuhoji endapo kodi wanazo lipa kupitia shughuli zao za kiuchumi zinaendana na huduma zinazo tolewa na serikali katika mitaa yao.


Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es Salaam Bi Rehema Madenge (mwenye ushungi) akiwasalimu washiriki wa mkutano wa viongozi wa JUWADA kabla haja mkaribisha Mgeni Rasmi Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makala kufungua mafunzo hayo Mei 03, 2023 katika ukumbi wa JNICC.

"Mwanamke kiasili anafanya mambo mengi zaidi katika jamii ikiwemo kusaidia malezi ya familia na pia katika shughuli za uchumi kwa kufanya ujasiriamali na serikali hua ina kusanya kodi katika biashara zao. Lakini, je? Huduma muhimu za kijamii anazo hitaji mwanamke mfano maji, gesi ya kupikia, matibabu nk vinapatikana kwa urahisi?" ameuliza Bi Gema Akilimali.

Amewataka viongozi wa JUWADA kusisitiza kuhusu wanawake kuhoji Bajeti za Kijinsia kwenye mitaa yao na kusema kufanya hivyo sio kuvunja sheria bali ni wajibu wao wa msingi kutetea haki zao.


Wakuu wa wilaya za mkoa wa Dar es Salaam walio hudhuria ufunguzi wa mkutano wa mafunzo ya viongozi wa JUWADA yaliyo fanyika jijini Dar Es Salaam Mei 03, 2023. Katikati mwenye tai ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule akiwa na wakuu wa wilaya wengine wawili wakimsikiliza Mgeni Rasmi Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akitoa hotuba yake (hayupo pichani)

Mafunzo hayo ya siku moja yalihudhuriwa pia na Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es Salaam (RAS DSM) Bi Rehema Madenge pamoja na wakuu wa wilaya za Kinondoni, Ilala, Kigamboni na Temeke pamoja na makatibu tawala wa wilaya hizo wakati wa ufunguzi. 


Pichani katikati ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Dar es Salaam (JUWADA) ambae pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1-TANZANIA Bi Fatuma Kange akiwa na Mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake Bi Gema Akilimali (kushoto) pamoja na mjumbe mwingine wa mkutano wa JUWADA (kulia) baada ya kumalizika mafunzo hayo ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam Mei 03, 2023.


Baadhi ya maofisa na watumishi wa benki ya CRDB ambao ndio walio fadhili na kuwezesha kufanyika kwa mafunzo hayo wakimsikiliza Mgeni Rasmi Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makala (hayupo pichani) wakati akitoa hotuba yake ya ufunguzi.


Wakufunzi walio toa mada za mafunzo mbalimbali katika mkutano huo wa mafunzo wa viongozi wa JUWADA wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makala mara baada ya kufungua mafunzo hayo. Taasisi zilizo toa mafunzo ni pamoja na Taasisi ya Uongozi, Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Women Fund Tanzania Trust, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, CRDB Bank, GS1-TANZANIA na IMBEJU.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments