Kaimu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Sengerema Makoye Sengerema. |
Na Anna Ruhasha, Mwanza.
Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya Sengerema mkoani Mwanza imeikataa taarifa ya shirika la umeme TANESCO wilayani humo kwa madai ya kutokidhi vigezo vya taarifa zinazotakiwa katika vikao vya madiwani .
Diwani wa kata ya Tabaruka Mhe Sospiter Busumabu akichangia hoja katika baraza la madiwani baada ya shirika la TANESCO kuwasilisha Taarifa. |
Hatua hiyo imekuja baada ya kutolewa hoja na diwani wa kata ya Tabaruka Sospiter Busumabu na kuungwa mkono na diwani wa kata ya Nyampande George Kazangu baada ya taarifa hiyo kuwasilishwa na kaimu Meneja wa TANESCO ambae hakutaka jina lake litajwe ambapo taarifa hiyo kukosekana saini ya Meneja TANESCO wilaya ya Sengerema.
Diwani wa halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza akichangia hoja kwenye kikao cha baraza la madiwani. |
Aidha,kaimu mwenyekiti wa halmashauri Mhe Makoye Sengerema alipoliuliza baraza la madiwani baada ya kaimu meneja kuwasilisha taarifa hiyo mbele ya kikao cha madiwani , baraza hilo liliikataa taarifa hiyo na kuagiza kwenda kuandaliwa taarifa nyingine itakayo wasilishwa kwenye kikao kijacho na kujadiliwa upya.
Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza |
Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza |
Mwisho.
0 Comments