Na Alphonce Kabilondo,Geita.
Mratibu wa dawati la uwezeshaji wanawake kiuchumi katika halmashauri ya mji Geita Mkoani hapa Valeria Makonda amesema kuwa majukwa ya wanawake ni sehemu maalum ya wanawake kusemea na kutatua kero zao na kuwaibua wanawake kutoka kwenye wimbi la umasikini.
Mratibu huyo ametoa kauli hiyo leo mei 15 mwaka huu kwenye uchaguzi wa viongozi wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi ngazi ya halmashauri ya mji uliofanyika kwenye ukumbi wa GEDECO mjini Geita .
Valeria Makonda, Mratibu wa dawati la uwezeshaji wanawake kiuchumi katika halmashauri ya mji Geita akiratibu zoezi la uchaguzi wa kupata viongozi wapya wa jukwaa la wanawake. |
Makonda amesema kuwa lengo la kuanzisha majukwa hayo ni kuwawezesha wanawake kupata sehemu maalumu ya kusemea changamoto zao na kuzitatua sambamba na kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kiuchumi hivyo viongozi waliochanguliwa wataliongoza jukwaa kwa kipindi cha miaka mitatu kwa mujibu wa sheria.
“Majukwaa haya yapo kwamujibu wa sheria, yameanzishwa kuanzia ngazi ya mitaa vijiji, kata na leo wamefanya uchaguzi ngazi ya halmashauri ya mji Geita na kuwapata viongozi watakao liongoza jukwaa kwa kipindi cha miaka mitatu" alisema Makonda .
Valeria Makonda - Mratibu wa dawati la uwezeshaji wanawake kiuchumi katika halmashauri ya mji Geita . |
Awali mwenyekiti wa uchaguzi huo Nyakaji Masaluli akitangaza matokeo hayo alitumia fursa hiyo kuwashauri wanawake hasa viongozi wapya waliochaguliwa kutooneana aibu wakati wa kutekeleza majukumu kwa kuwachukulia hatua ikiwemo kuwafukuza au kuwaondoa katika nafasi watakaoonekana kuzembea kwa namna yoyote.
Mwenyekiti huyo wa uchaguzi alitangaza matokeo huku akiwataja viongozi walio chaguliwa kwenye uchaguzi huo kwa majina yao na nafasi walizo shinda, ambapo nafasi ya mwenyekiti aliyeshinda na kutangazwa rasmi ni Onester Madata, makamu mwenyekiti Joyce Luchungulila.
Aidha wengine waliochaguliwa na kutangazwa rasmi kuwa washindi ni katibu mkuu Jenipha Paschal huku katibu msaidizi akiwa ni Rachel Jumbe, mwekahazina ni Conchester Kazaula pamoja na wajumbe watatu wa jukwaa hilo ambao ni Jesca Masota, Halima Masele na Pendo Mawaya.
Mwenyekiti wa dawati la uwezeshaji wanawake kiuchumi katika halmashauri ya mji Geita ni Onester Madata (kushoto) na makamu wake ni Joyce Luchungulila (kulia-gauni rangi nyekundu) |
Wajumbe watatu wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi katika halmashauri ya mji Geita ni Jesca Masota (mwenye miwani) Halima Masele (anaye andika) na Pendo Mawaya ( aliyeshika mkoba). |
Wagombea nafasi ya Katibu wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi halmashauri ya mji Geita wakipigiwa kura. |
Wanawake wa jukwaa la uwezeshaji kiuchumi halmashauri ya mji Geita wakifanya uchaguzi wa viongozi wao leo 15 Mei 2023. |
Mwisho.
0 Comments