TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

WAANDISHI WAKUMBUSHWA KUZINGATIA MAADILI YAO YA KAZI

Mhe Cornel Magembe (Mkuu wa wilaya Geita) akitoa hotuba kwenye maadhimisho ya siku ya UHURU wa vyombo vya habari Duniani katika ngazi ya mkoa mkoani Geita, kulia kwake ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita ACP.Safia Jongo . 

Na Alphonce Kabilondo, Geita. 

Mkuu wa wilaya Geita mkoani hapa Cornel Magembe amewataka waandishi wa habari kuandika habari kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao na kutangaza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.

Mkuu huyo  ametoa kauli hiyo jana alipokuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya UHURU wa vyombo vya habari Duniani ambayo hufanyika mei 3 kila mwaka na kimkoa sherehe hiyo imefanyika katika ukumbi wa bwalo la Polisi 24 Mei 2023.

Cornel Magembe Mkuu wa wilaya Geita akihutubia kongamano la maadhimisho ya siku ya UHURU wa vyombo vya habari Duniani kwa mkoa wa Geita (aliyesimama), kushoto kwake ni Renatus Masuguliko (Mwenyekiti GPC) na kulia kwake ni ACP Safia Jongo (RPC Geita) na ACP Amon Mimata (Operation Officer Geita).

Magembe amesema kuwa waandishi wa habari ni watu muhimu wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kuelimisha, na kuhabarisha umma licha ya kufanya kazi katika mazingira magumu sana.

Alisema anatamani katika maboresho ya sheria ya habari kuona vyombo vya habari vinatambulika kama muhimili wa nne katika mihimili ya serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

" Nawapenda sana waandishi wa habari, viongozi tunateuliwa hatuna chuo lakini ukiangalia vyombo vya habari mbali mbali unapata elimu hivyo endeleeni kutoa elimu kwa kuzingatia maadili yenu." Alisema mkuu huyo.

Akisisitiza kauli hiyo alisema kuwa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Geita ndio sehemu pekee ya kuwaleta pamoja waandishi wa habari kujadili na kutatua changamoto zao, huku akiongeza kuwa serikali inatambua mchango wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Geita (Geita Press Club-GPC) katika maendeleo ya Geita.

Cornel Magembe (DC Geita) akiwasha piki piki ishara ya kuzindua rasmi mradi wa piki piki wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Geita Mei 24, 2023 siku ya Media Day. 

Pia akizindua mradi wa piki piki wa Klabu hiyo aliwapongeza viongozi na wanachama wa Geita Press Club-GPC kwa kuanzisha wazo la kuwa na mradi wa kitega uchumi, na hivyo kuwaunga mkono kwa kuwaongezea piki piki nyingine moja ili ziwe mbili walau mradi huo usaidie kuingiza kipato kwa manufaa ya waandishi wote. 

Cornel Magembe Mkuu wa wilaya Geita (katikati) akimkabidhi kadi ya pikipiki Bw.Renatus Masuguliko (Mwenyekiti-GPC) kwa niaba ya Waandishi wa habari mkoa wa Geita baada ya kuzindua rasmi mradi wa piki piki, upande wa kushoto ni Novatus Lyaruu (Katibu Mkuu Mtendaji GPC)

Aidha kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Geita ACP. Safia Jongo akatumia fursa hiyo kuwahimiza waandishi wa habari ambao bado hawajajiunga na Geita Press Club-GPC kufanya hivyo ili waweze kunufaika na fursa za mafunzo ya kimaadili na kufanya kazi kwa weledi.

Pichani aliyesimama ni ACP Safia Jongo (RPC Geita) akiwasisitiza waandishi wa habari mkoani Geita kujiunga na Geita Press Club-GPC ili kunufaika na fursa zinazopatikana kupitia klabu hiyo. Kulia kwake ni ACP Amon Mimata (OPER-Officer Geita), Asi Oyugi (Afisa Uhamiaji Geita) na Godfrey Odupoy (Mwendesha mashtaka Geita).

Pia alikemea kuandika habari zisizo sahihi ambazo zimekuwa zikichangia kuibua taharuki kwa jamii akitolea mfano tukio la uwongo lililoripotiwa na baadhi ya waandishi  juu ya kuwepo kwa kaburi la mtoto mdogo kufukuliwa na mwili wake kuchukuliwa, kitendo ambacho si kweli.

Baadhi ya washiriki kwenye maadhimisho ya siku ya UHURU wa vyombo vya habari Duniani kwa mkoa wa Geita, anaeonekana kwa karibu ni Afande Fidelis Ngonyani (Zimamoto Geita).

Nae muwakilishi wa Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Geita Azza E. Mtaita alisema bila kukemea vitendo vya rushwa klabu ya waandishi wa habari haiwezi kusonga mbele.

"Waandishi timizeni wajibu wenu, tufanye kazi kwa pamoja na kufichua viashiria vya rushwa" alisema Mtaita.

Katika picha ni Azza E . Mtaita (DRBC -TAKUKURU Geita) akitoa mada kwenye maadhimisho ya siku ya UHURU wa vyombo vya habari Duniani kwa mkoa wa Geita Mei 24,2023.

Awali katibu mkuu mtendaji wa Geita Press Club-GPC Novatus Lyaruu akisoma risala kwa mgeni rasmi alisema klabu hiyo inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vitendea kazi ikiwemo kamera, kompyuta na samani za ofisini.

Katibu Mkuu Mtendaji wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Geita Novatus Lyaruu akisoma risala kwa mgeni rasmi Mkuu wa wilaya Geita kwenye siku ya Media Day. 

Pia aliongeza kuwa klabu hiyo imefanikiwa kununua kiwanja kwaajili ya ujenzi wa ofisini katika eneo la Kanyala halmashauri ya mji Geita na piki piki moja aina ya SANLG kwaajili ya kuanzisha mradi wa boda boda ili kuondokana na hali ya utegemezi.

Novatus Lyaruu Katibu Mkuu Mtendaji GPC akisoma risala kwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya UHURU wa vyombo vya habari Duniani kwa mkoa wa Geita. 

Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari (Geita Press Club-GPC) Renatus Masuguliko akifunga maadhimisho hayo alisema kuwa klabu pekee mkoani hapa inayotambulika kisheria na ni mwanachama wa Muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs-UTPC) na Baraza la habari Tanzania (Media Council of Tanzania-MCT).

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Geita Bw. Renatus Masuguliko akishukuru wadau wa habari waliohudhuria kwenye maadhimisho ya siku ya UHURU wa vyombo vya habari Duniani kwa ngazi ya mkoa hususan Mgeni rasmi Cornel Magembe Mkuu wa wilaya Geita na wakuu wa taasisi wote. 

Mwenyekiti huyo alisema klabu hiyo itaendelea kusimamia waandishi wote wanachama na wasiokuwa wanachama kuandika habari kwa kuzingatia maadili na kwa weledi wa hali ya juu bila kuegemea upanda wowote. 

Renatus Masuguliko Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Geita akitoa salamu za klabu hiyo kwa wadau wa habari wakati akifunga hafla ya Media Day mkoani Geita 24 Mei 2023.

Michael Bundala (aliyesimama) Mwandishi wa habari Rubondo FM radio akichangia hoja kwenye maadhimisho ya Media Day mkoani Geita. 

 Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ya "Kuunda mustakabali wa haki, UHURU wa kujieleza kama kichocheo cha haki nyingine zote za binadamu"  yamehudhuriwa na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari kutoka wilaya zote tano za mkoa wa Geita ambazo ni Bukombe, Mbogwe, Chato, Nyang'hwale na Geita pamoja na viongozi wa taasisi za serikali, vyama vya siasa na viongozi wa madhehebu ya dini. 

ACP Amon Mimata (Operation Officer Geita)akitoa mada kwa Waandishi wa habari mkoa wa Geita. 



Angel G. Sembony kutoka Ofisi ya GEUWASA Geita (PRO)akiwasilisha mada kwenye maadhimisho ya siku ya UHURU wa vyombo vya habari Duniani kwa mkoa wa Geita 


INSP. Edward Lukuba (Zimamoto Geita) akitoa mafunzo kwa Wanahabari na wadau wa habari juu ya namna ya kujikinga na kukabiliana na majanga ya moto. 
Calystus Mpangala kutoka ofisi ya NHIF Geita (RM) akitoa mada kwenye maadhimisho ya siku ya UHURU wa vyombo vya habari Duniani katika ngazi ya mkoa mkoani Geita. 
Asi Athanas Oyugi kutoka ofisi ya Uhamiaji mkoa wa Geita akitoa mada kwa wanahabari na wadau wa habari waliohudhuria maadhimisho ya siku ya UHURU wa vyombo vya habari Duniani kwa mkoa wa Geita. 
Fidelis Ngonyani kutoka Jeshi la Zimamoto Geita akifundisha kwa vitendo namna ya kukabiliana na majanga ya moto kwa washiriki wa maadhimisho ya siku ya UHURU wa vyombo vya habari Duniani kwa mkoa wa Geita 
Samweli Masunzu Mwandishi wa habari Radio Kwizera FM akijifunza kwa vitendo kuzima moto kwa niaba ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Geita katika kuadhimisha Media Day. 

Godfrey Odupoy kutoka Ofisi ya mwendesha mashtaka mkoa wa Geita akiwasilisha mada kwenye maadhimisho ya siku ya UHURU wa vyombo vya habari Duniani kwa mkoa wa Geita 24/5/2023.


Mgeni rasmi Cornel Magembe (DC Geita) alievalia suti ya bluu katikati akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mkoa wa Geita, kushoto kwake ni ACP Safia Jongo (RPC Geita) na kulia kwake ni Renatus Masuguliko (Mwenyekiti-GPC ).




Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments