|
Mlezi wa Utume wa Wana Taaluma Wakatoliki Tanzania katika Jimbo Katoliki laDSM (Catholic Professionals of Tanzania-CPT) Padre Victor Missien akiongea na viongozi wa CPT Jimbo la DSM kwenye Ukumbi wa Parokia ya Manzese leo Mei 13, 2023 kabla ya kufanyika uchaguzi wa viongozi wapya wa Kamati Tendaji ya CPT Jimbo la DSM. |
Na Urban Epimark, DSM
Mlezi wa Utume wa CPT Jimbo Katoliki la DSM Padre Victor Missien amewataka wanataaluma mbalimbali katika Jimbo la DSM kuwa tayari kutumia taaluma na vipawa vyao kulitumikia kanisa ikiwa ni wajibu wao kama wabatizwa.
Pia Mlezi huyo ametoa rai kwa viongozi wote wa Utume wa CPT katika Jimbo Katoliki la DSM kuwaelezea kwa ufasaha mapadre na maaskofu kwenye maeneo yao kuhusu malengo na umuhimu wa CPT ili waweze kuwatumia katika mipango yao katika kuwasaidia waamini kwa mambo mbalimbali.
Padre Missien ameyasema hayo leo Mei 13, 2023 muda mfupi mara baada ya kumalizika mkutano wa uchaguzi wa viongozi wapya wa Kamati Tendaji ya CPT Jimbo la DSM uliofanyika Parokia ya Manzese.
|
Msimamizi wa Uchaguzi wa Viongozi wa Utume wa CPT Jimbo la DSM ambae ni Naibu Katibu wa Kamati ya Uinjilishaji Jimbo la DSM na pia Katibu wa Halmashauri ya Walei Parokia ya Mt Augustino Salasala Bi Scolastica Mandwa akielezea taratibu za uchaguzi kwa wajumbe wa mkutano huo muda mfupi kabla hawajaanza kufanya uchaguzi huo katika ukumbi wa Parokia ya Manzese leo Mei 13, 2023. Mwanzo kulia ni Mratibu wa CPT Jimbo la DSM ambae pia ni Mratibu wa CPT Taifa Bi Mariam Kessy. |
Nae Msimamizi wa Uchaguzi huo ambae ni Naibu Katibu wa Kamati ya Uinjilishaji Jimbo Katoliki la DSM lakini pia ni Katibu wa Halmashauri ya Walei Parokia ya Mt Augustino Salasala Bi Scolastica Mandwa aliwasomea wajumbe sehemu ya maandiko matakatifu kutoka waraka wa kwanza wa Mtume Petro (1Petro5:1-4) kuhusu viongozi hao kujitoa kikamilifu kulichunga kundi la Mungu kupitia Utume wa CPT.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya viongozi walio chaguliwa, Mwenyekiti mteule wa CPT Jimbo la DSM Bw Thomas Brash aliwashukuru wajumbe kwa kuwachagua na kusema kazi ya kuijenga CPT sio ya muda mfupi bali itawachukua muda mrefu hivyo wana CPT wasikate tamaa bali wazidi kumtumainia Mungu Roho Mtakatifu awaongoze kutimiza Utume wao.
|
Sehemu ya wajumbe wa mkutano wa uchaguzi wa CPT Jimbo la DSM wakimsikiliza Mlezi wa CPT Jimbo la DSM Padre Victor Missien (hayupo pichani) akitoa hotuba yake kabla ya kufanyika uchaguzi wa viongozi wa Kamati Tendaji ya CPT Jimbo la DSM uliofanyika ukumbi wa Parokia ya Manzese leo Mei 13, 2023. |
|
Viongozi wapya wateule wa Kamati Tendaji ya CPT Jimbo la DSM wakiwa katika picha ya pamoja na Mlezi wao Padre Victor Missien (shati jeupe) na kufutiwa na Msimamizi wa Uchaguzi huo Bi Scolastica Mandwa (wa pili kushoto). Viongozi wapya na majina na parokia wanako toka, kuanzia kulia ni Katibu wa CPT ambae kitaaluma ni Mwalimu, Bw Edward Ludengama kutoka parokia ya Kwembe. Anafuatiwa na Mwenyekiti wa CPT Jimbo, kitaaluma ni Mwanasheria Bw Thomas Brash (aliye shika kitabu) kutoka parokia ya Mavurunza na kulia kwake ni Makamu M/k wa CPT Jimbo, kitaaluma ni Daktari wa watu, Dr Getrude Kahumba kutoka parokia ya Mbezi Mshikamano. Mwingine kutoka kushoto ni Naibu Katibu wa CPT Jimbo, ambae kitaaluma ni Mwalimu Bw Peter George anae toka pia parokia ya Mbezi Mshikamano. |
Mwisho.
0 Comments