Na. Samwel Masunzu Geita
Bukombe, Geita
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2024 kitaifa Godfrey
Mnzava ametembelea shule ya msingi yenye wanafunzi wenye mahtaji maalumu
ya Ushirombo wilayani Bukombe mkoani Geita na kukabidhi vifaa vya
kujifunzia kwa wanafunzi 385.
Mwenge wa uhuru umefika kwenye shule hiyo kukagua
maendeelo ya mradi wa shule hiyo yenye wanafunzi wenye mahtaji maalumu
wanaosoma shuleni hapo.
Kiongozi wa mbio za mwenge Mnzava amekabidhi madafari, kalamu,
cherehani pamoja na masweta vitakavyowasaidia wanafunzi wa shule hiyo wakati wa
kujifunza.
Mnzava pia ametembelea bustani ya mboga mboga ambayo iliandaliwa na wanafunzi wa shule hiyo kwaajili ya kupata lishe bora na kupongeza jitihada za walimu katika kutoa malezi kwa watoto hao.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo maalumu elimu maalumu wilaya ya
Bukombe Joyce Mangi amesema shule hiyo ina wanafunzi 385 wavulana wakiwa ni 192
na wasichana wakiwa ni 193.
Mangi amesema kati ya wanafunzi hao, 116 wana ulemavu wa akili,
54 ni viziwi 155 wana ulemavu wa viungo na 15 wana ualbino
Mwenge wa uhuru Oktoba 2 umewasili wilayani Mbogwe
mkoani Geita ambapo utapitia miradi 9 yenye thamani ya shilingi bilioni 4
Mkuu wa wilaya ya Bukombe Paskasi Buragili ameukabidhi mwenge
kwa mkuu wa wilaya ya Mbogwe Sakina Mohamed.
Mwisho
0 Comments