TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

SERIKALI YAFUTA LESENI ZAIDI YA 2,000 ZA UCHIMBAJI MADINI, KUGAWA MAENEO KWA WACHIMBAJI WADOGO.

Na Samwel Masunzu: 

Serikali kupitia Wizara ya Madini imefuta zaidi ya leseni 2,000 za uchimbaji madini zilizokuwa zikimilikiwa na wachache, hatua iliyolenga kuwaruhusu wachimbaji wadogo kupata maeneo ya kuchimba madini.

Waziri wa madini, Anthony Mavunde, amethibitisha hatua hiyo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Nyakafulu, wilayani Mbogwe, mkoani Geita. Akiwa katika ziara hiyo, Waziri Mavunde alitembelea na kuweka mawe ya msingi kwenye kituo cha afya cha ushirika na hospitali ya wilaya ya Mbogwe.

Mavunde alisema kuwa baada ya serikali kuchukua maeneo hayo, zoezi la kugawa upya maeneo hayo kwa wachimbaji wadogo litaanza mara moja.

“Leseni za uchimbaji zitatolewa kwa vikundi ili kuhakikisha kila mmoja mwenye uwezo wa kuchimba madini anapata fursa ya kufanya hivyo.” Mavunde

Mwisho.


Waziri wa madini, Anthony Mavunde, 

Post a Comment

0 Comments