TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

VIJANA NDIO WENYENCHI: JIANDIKISHENI KUPIGA KURA


Mzee Ahmadi Saidi Ndege (81) akiwa na mwanahabari nyumbani kwake katika kitongoji cha Keko kijiji cha Majengo wilayani Tandahimba mkoani Mtwara akitoa maoni yake juu ya mwenendo wa vijana wa leo. 
Na Beatus Bihigi - Mtwara.

Mzee Ndege mwenye umri wa miaka 81 mkazi wa kijiji cha Majengo Tandahimba ameonesha kuwashangaa vijana wa leo kwa jinsi ambavyo wanasua sua katika kutumia haki yao ya kikatiba ya kujiandikisha kwenye daftari la mkazi ili kuweza kupiga kura kuchagua viongozi wao wa mamlaka za serikali za mitaa.

Mzee Ahmadi Saidi Ndege (81) akiwaasa vijana kujitokeza kujiandikisha kwaajili ya kupiga kura kuwachagua viongozi wao wa mamlaka za serikali za mitaa 

"Mimi nawashangaa vijana kusuasua kujiandikisha wakati hii nchi ni yao sisi tumeshazeeka, niwazembe" alisema Mzee Ndege.

Wakati akihojiwa na mwandishi wa habari amesema serikali imefanya vizuri sana kuwaleta waandikishaji wa wapiga kura kwenye kila kitongoji ili kila mwenye sifa ajiandikishe aweze kupiga kura.

Ahmadi Saidi Ndege (81) akiwahamasisha wakazi wa kitongoji chake anachoishi Keko kuendelea kujitokeza kujiandikisha ili waweze kupiga kura 

Anaipongeza serikali kwa jitihada zake za kuwaletea maendeleo huku kusini, anamshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea huduma za jamii ikiwemo hospitali,  shule, maji na umeme.

Mzee Ndege akiwa na mgeni wake mwanahabari 

Nae Mzee Hamisi Adam Nanyanga (73) akitoa maoni yake juu ya vijana na zoezi la kujiandikisha amesema vijana wengi wanapuuzia kwa makusudi kufika kwenye vituo kujiandikisha lakini kwa upande mwingine alikiri kuwa vijana wako kwenye harakati za biashara ya korosho ambapo anamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa bei nzuri ya zao hilo mkombozi kwa mkoa wa Mtwara. 

Mzee Hamisi Adam Nanyanga (73) akizungumza na mwandishi wa gazeti hili, akiwahamasisha wananchi wa kata ya Mndumbwe kijiji cha Majengo Tandahimba wajitokeze kujiandikisha. 

Mzee Hamisi Adam Nanyanga mkazi wa Tandahimba mkoani Mtwara akiwaomba wananchi kuendelea kujiandikisha ili kuchagua viongozi wao wa serikali za mitaa 


Mwisho. 


Post a Comment

0 Comments