TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

WAZIRI WA MADINI, ANTHONY MAVUNDE, ATOA MAAGIZO WILAYA YA MBOGWE KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO KWA UFANISI.

Na Theresia C Method:

Waziri wa madini, Anthony Mavunde, ameutaka uongozi wa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kuhakikisha wanasimamia kwa ufanisi fedha zilizotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kunufaisha wananchi.

Mavunde ametoa maagizo hayo wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha afya cha kata ya Ushirika wilayani Mbogwe. Ujenzi wa kituo hicho, ambao unagharimu zaidi ya shilingi milioni 500, umekuwa ukisuasua kutokana na changamoto za usimamizi wa awali, hali iliyopelekea Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuingilia kati na kuchukua hatua dhidi ya wasimamizi wa mradi.

Mbunge wa jimbo la Mbogwe, Nikodemas Maganga, pamoja na diwani wa kata ya Ushirika, Mrisho, wamepongeza hatua zilizochukuliwa, wakisema kuwa zitaleta msukumo katika kukamilisha ujenzi wa kituo hicho kwa wakati.

 Baadhi ya wananchi wa kata hiyo wameeleza kuwa kukamilika kwa kituo hicho cha afya kutapunguza changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.

Katika ziara yake, waziri Mavunde ametembelea na kuweka mawe ya msingi kwenye kituo cha afya cha Ushirika na hospitali ya wilaya ya Mbogwe. Pia alifanya mkutano wa hadhara katika Kata ya Nyakafulu ambapo alieleza kuwa serikali, katika kipindi cha miaka mitatu, imetoa zaidi ya shilingi bilioni 800 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mwisho


                                      Waziri wa madini, Anthony Mavunde

Post a Comment

0 Comments