|
Rev. Stevie Robert Mlenga: Askofu Mkuu wa kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania -FPCT |
Askofu Mkuu wa kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT) Rev. Stevie Mulenga kwa njia ya simu amezungumza na viongozi wa ngazi za juu wa kanisa hilo katika jimbo la kusini (Mtwara) wakiwa katika kikao maalum cha utendaji kuelekea zoezi la uchaguzi unatarajiwa kufanyika 30/11/2024 kupata viongozi wa jimbo hilo.
|
Pichani kushoto kwako ni Francis J. Chiwango (Askofu wa kanisa la FPCT jimbo la kusini- Mtwara) na upande wa kulia ni Chigogolo Mohamed (Katibu Mkuu wa FPCT jimbo la kusini yaani mkoa wa Mtwara) |
"Sasa ninyi siyo jimbo la kimkakati tena, mnapaswa kufuata kanuni, taratibu na miongozo yote ya uchaguzi ili kuwapata viongozi wenu" alisema Askofu Mlenga.
Aliongeza kusema kuwa pale inapo hitajika kutumia hekima hekima hiyo itumike chini ya usimamizi na maelekezo ya Askofu wa jimbo la Mtwara anayemaliza muda wake Rev. Francis J. Chiwango.
|
Katika picha ni Rev. Francis J. Chiwango (kushoto) Askofu wa jimbo la kusini wa kanisa la FPCT akitoa neno la utangulizi na kufungua kikao cha wachungaji viongozi na makatibu wa makanisa ya mahali leo mapema katika kanisa la FPCT Mnazimmoja Lindi na pembeni yake ni Rev. M Chigogolo Mohamed (Katibu wa jimbo la kusini FPCT) akiandika nukuu za kikao hicho leo 02 Novemba 2024. |
Askofu Mkuu Rev. Mlenga alisisitiza juu ya kumtumikia Mungu kama wito na asiwepo mtu akadhani wito wake ni kuwa Askofu wa jimbo au Katibu, ila Mungu aonaye sirini akiona vema mtu apate nafasi hiyo anaweza kupata nafasi hizo za uongozi na waliobaki watoe ushirikiano kwa viongozi watakao chaguliwa ili kufanya kazi ya Mungu. Aliwatakia uchaguzi mwema na Rohomtakatifu atawale.
|
Pichani ni baadhi ya wachungaji viongozi na makatibu wa makanisa ya mahali FPCT jimbo la kusini wakiwa kwenye kikao cha jimbo mapema leo 02/11/2024 |
Kikao hicho kimefanyika leo 02 Novemba 2024 katika kanisa la FPCT Mnazimmoja mkoani Lindi, na kuhudhuriwa na wachungaji viongozi na makatibu watendaji wa makanisa ya mahali yote Saba ikiwemo kanisa la mahali Newala linaloundwa na wilaya mbili Newala na Tandahimba.
|
Katika picha walioketi mustari wa mbele wa kwanza kushoto ni makamu Askofu wa jimbo la kusini Rev. Erasto S. Kambona akiwa na wajumbe wengine wa kikao hicho kilichofanyika katika kanisa la FPCT Mnazimmoja Lindi leo 02/11/2024 |
|
Wachungaji viongozi na makatibu wa makanisa ya mahali yasiyo pungua sita na yasiyo zidi saba (7) wakiwa katika kikao cha jimbo kilichoandaliwa na kuitishwa na Askofu Francis J. Chiwango wa FPCT jimbo la kusini. |
|
Baadhi ya wajumbe wa kikao, ambao ni wachungaji na makatibu kutoka makanisa ya mahali ya FPCT jimbo la kusini (Mtwara) wakiwa katika kikao cha kiutendaji Mnazimmoja Lindi. |
|
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha jimbo wakiwa kwenye kikao cha ngazi ya juu cha kanisa la FPCT leo tarehe 2/11/2024. Mjumbe aliyefunga tai ni Beatus S. Bihigi -BED PPM (Katibu Mkuu Mtendaji wa kanisa la mahali FPCT Newala) akiwa miongoni mwawajumbe waliohudhuria kikao hicho muhimu. |
|
Pichani ni wachungaji viongozi (Senior Pastors) wa makanisa ya mahali jimbo la kusini Mtwara wakiwa kwenye kikao. Aliye valia suti nyeusi wakwanza kulia na anayeonekana kuandika jambo flani kwenye kikao hicho ni Rev. Anthony Peter Mbajije, Mchungaji kiongozi wa kanisa la mahali Newala. |
|
Walioketi katika picha ni Askofu Francis J. Chiwango (katikati), kulia kwake ni Makamu Askofu Erasto S. Kambona na upande wa kushoto kwake ni Katibu wa jimbo Rev. Chigogolo Mohamed na waliosimama ni wachungaji na makatibu wa makanisa ya mahali (Local churches) FPCT jimbo la kusini wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa jimbo baada ya kikao. |
|
Walioketi katika picha ni Askofu Francis J. Chiwango (katikati), kulia kwake ni Makamu Askofu Erasto S. Kambona na upande wa kushoto kwake ni Katibu wa jimbo Rev. Chigogolo Mohamed na waliosimama ni wachungaji na makatibu wa makanisa ya mahali (Local churches) FPCT jimbo la kusini wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa jimbo baada ya kikao leo 02/11/2024. |
Mwisho.
0 Comments