Na mwandishi wetu;
Katika kuadhimisha siku 16 za kupinga
ukatili wa kijinsia, leo November 25, 2024 kumefanyika maandamano ya amani ya
kupinga ukatili katika mkoa wa Manyara.
Maandamano hayo yamafanyika asubuhi ya leo ambayo yameanzia katika viwanja vya stendi ya zamani iliyoko katika mji wa Babati hadi katika ukumbi wa white rose ambapo waandamanaji wametembea kwa zaidi ya km 10.
Maandamano hayo yamewashirikisha makundi mabalimbali wakiwemo wafanyabiashara wa mkoa wa Manyara, waandishi wa habari, wanavyuo, maaafisa usafirishaji na wadau mbalimbali.
Aidha, maandamano hayo yameandaliwa
na umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC), klabu ya waandishi wa
habari mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Manyara kwa
lengo la kusambaza ujumbe katika jamii wa kupinga vitendo vya ukatili.
0 Comments