TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

WANANCHI WAPEWA FIDIA YA BILIONI 7 NA BARRICK - BULYANHULU BAADA YA KERO YA TAKUKURU RAFIKI

 Na Theresia C Method:



Wananchi 226 wa kata ya Mwingiro wilayani Nyang'hwale wamelipwa fidia ya jumla ya shilingi 7,206,991,048 na mgodi wa Barrick - Bulyanhulu baada ya kero yao kuibuliwa katika kikao cha TAKUKURU Rafiki mnamo februari 21, 2023. Katika kikao hicho, wadau walilalamikia mgodi huo kwa kuchukua maeneo yao kwa zaidi ya miaka 20 kwa ajili ya utafiti wa madini bila malipo ya fidia.

TAKUKURU ilipopeleka malalamiko hayo kwa mgodi wa Barrick, tathmini ya fidia ilifanyika mnamo novemba 2023, na fidia imelipwa kwa wananchi wote ifikapo agosti 23, 2024. Hatua hii ni sehemu ya jitihada za TAKUKURU katika kufuatilia na kutatua kero zinazoweza kuchochea vitendo vya rushwa.

Kipindi cha julai hadi septemba 2024, TAKUKURU Rafiki imezifikia kata 10 ambapo kero 56 ziliibuliwa. Kero 34 zilipatiwa majibu, na kero 22 zimewasilishwa kwa watoa huduma ili kupata ufumbuzi wa kudumu. TAKUKURU inatarajia kushirikiana na idara husika kutoa mrejesho kwa wananchi waliotoa kero hizo.

Pia, TAKUKURU kupitia Dawati la Udhibiti na Uzuiaji Rushwa, imefanya ufuatiliaji wa miradi 26 yenye thamani ya jumla ya shilingi 9,648,033,262.19. Miradi hii ni pamoja na sekta ya elimu (shilingi 5,517,012,930.68), maji (shilingi 3,586,866,305.74), na afya (shilingi 544,154,025.77). Miradi 13 ilionekana kuwa na mapungufu, na ushauri umetolewa kurekebisha mapungufu hayo.

Hata hivyo, TAKUKURU imebaini miradi mitatu yenye thamani ya shilingi 2,984,145,403.95 ambayo ina mapungufu makubwa katika matumizi ya fedha, na hatua za uchunguzi zinaendelea.


 

 


Post a Comment

0 Comments