TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

MHE. DC KANALI MNTENJELE AWATOA HOFU WAKAZI WA MNDUMBWE TANDAHIMBA KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA UHURU WA TANGANYIKA DISEMBA 9


Mhe. Kanali Michael Mntenjele Mkuu wa wilaya Tandahimba katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Tanganyika amewatembelea na kuzungumza na baadhi ya wahanga ambao nyumba zao zimebomoka kufuatia  mvua kubwa iliyoambatana na Upepo mkali katika kata ya Mndumbwe. 

Na; Beatus Bihigi - Mtwara Tanzania. 
Mkuu wa wilaya Tandahimba Mhe. Kanali Michael Mntenjele katika kuadhimisha sherehe za Uhuru wa Tanganyika leo Disemba 9, ame watembelea wananchi wa kijiji na kata ya Mndumbwe tarafa ya Mambamba wilayani humo kuwapa pole kufuatia makazi yao hususani nyumba za kuishi kubomoka kabisa na nyingine kuezuliwa paa zake kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha jana jioni Disemba 8,2024.
Nyumba iliyobomoka na kuangushwa na upepo mkali katika kijiji cha Mndumbwe kata ya Mndumbwe tarafani Mambamba wilayani Tandahimba mkoani Mtwara Tanzania 

Mkuu wa wilaya Mhe Kanali Mntenjele aliwatia moyo wananchi hao wasiwe na hofu huku akitumia siku hii pia ya Uhuru kuwakumbusha wazazi wenye watoto wa umri wa kuanza shule na wale waliofaulu kujiunga na sekondari kufanya maandalizi ya  kuwaandikisha darasa la awali na lakwanza na wale wa sekondari kuwapeleka shuleni ifikapo Januari 13, 2025. 

Mhe Kanali Michael Mntenjele Mkuu wa wilaya Tandahimba akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mndumbwe kata ya Mndumbwe tarafa ya Mambamba wilayani humo kufuatia nyumba zipatazo 35 kuezuliwa na upepo mkali. 


Mkuu wa wilaya huyo akiwa ameambatana na Maofisa kutoka Ofisini kwake wakiwemo wa vyombo vya ulinzi na usalama walifika kushuhudia uharibifu huo ambao umewaacha baadhi ya wakazi katika kijiji na kata hiyo ya Mndumbwe bila makazi ya kuishi.
Nyumba iliyobomoka katika kijiji cha Mndumbwe Tandahimba kutokana na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa. 

Aidha katika taarifa iliyotolewa na viongozi wa serikali ya kijiji cha Mndumbwe ambacho hasa ndicho kilichoathirika na upepo huo, wamesema nyumba 35 zime bomolewa huku ikiwa ni nyumba 4 tu ambazo ziliezuliwa paa, ukuta  ukibakia salama, lakini nyumba zilizosalia thelathini na moja (31) zipo katika hali mbaya sana kwani paa zimeezuliwa na kuta za nyumba hizo kuporomoka na kubomoka kabisa pasiwepo namna yoyote ya kuzirekebisha zaidi ya kujengwa kwa upya. 
Nyumba iliyobomoka katika kijiji cha Mndumbwe Tandahimba kutokana na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa


Nyumba iliyoezuliwa paa katika kijiji cha Mndumbwe Tandahimba kutokana na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa


Baadhi ya kinamama na watoto wakiwa wamehamaki kilichotokea ambapo nyumba zao zimebomoka na kuezuliwa paa katika kijiji cha Mndumbwe Tandahimba Mtwara. 

Pia Mhe Kanali Mntenjele amewaasa wananchi hao kutojihusisha na mambo yasiyo faa ikiwemo kuepuka mikopo yenye riba kubwa almaarufu kama kausha damu na vitendo vya ushirikina vyakuwategemea waganga wa kienyeji kwani serikali ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejenga zahanati, Vituo vya afya na hospitali karibu kila mahali nchini kote hivyo wavitumie kwa kupata matibabu. 

Mhe. Kanali Michael Mntenjele Mkuu wa wilaya Tandahimba katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Tanganyika leo Disemba 9, amewatembelea na kuzungumza na baadhi ya wahanga ambao nyumba zao zimebomoka kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na Upepo mkali katika kata ya Mndumbwe. 

Nyumba iliyobomoka Disemba 8, kuamkia leo Disemba 9,2024 katika kijiji cha Mndumbwe kata ya Mndumbwe wilayani Tandahimba mkoani Mtwara. 

Wakazi wa kijiji cha Mndumbwe wameonesha kusikitishwa na hali hiyo huku wasijue chakufanya kwa sasa ili kuwasaidia wale ambao nyumba zao zimeanguka chini.

Mwisho. 

Post a Comment

2 Comments