TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

MNDUMBWE YAJIANDAA NA UMISSETA

Pichani ni Mkuu wa shule ya sekondari Mndumbwe Ntarisa K. Ntarisa (aliyevaa shati nyeupe, akiwa katikati) akimkabidhi jezi Mwalimu wa michezo katika shule hiyo Bi. Mwansite W. Shali mbele ya Wanafunzi viranja wa michezo Ofisini kwake leo 6/2/2025

 Na; Beatus Bihigi - Mtwara

Mkuu wa shule ya sekondari Mndumbwe iliyopo wilayani Tandahimba mkoani  Mtwara Bw. Ntarisa K. Ntarisa leo tarehe 6 February 2025 amemkabidhi Mwalimu wa michezo Bi. Mwansite W. Shali jezi za mchezo wa mpira wa miguu (Football jersey) na mpira wa mikono (Netball jersey) ikiwa ni hatua ya maandalizi ya kushiriki katika Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) kwa mwaka 2025/26.

Ntarisa K . Ntarisa Mkuu wa shule ya sekondari Mndumbwe akiwa katika zoezi la kukabidhi vifaa vya michezo kwa walimu na Wanafunzi wa idara ya michezo shuleni hapo leo 6/2/2025

Aidha Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Ntarisa K. Ntarisa ameahidi kuendelea kusimamia suala la michezo kikamilifu, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mahitaji yote ya idara ya michezo shuleni hapo yanakamilika. "Kwa jezi za mpira wa mikono yaani netball nimekubali ombi lenu la kuongeza suruali ndefu za michezo" alisema Mkuu huyo.

Mkuu wa shule ya sekondari Mndumbwe wilayani Tandahimba mkoani Mtwara Mwalimu Ntarisa K. Ntarisa akiwahakikishia idara ya michezo shuleni hapo kuwa Ofisi yake inaingalia idara hiyo kwa jicho la tatu kama ilivyo kwa idara nyingine zote shuleni hapo. 

Nae Mwalimu wa michezo katika shule hiyo kwa niaba ya Mwalimu mwenake katika idara hiyo na kwaniaba ya walimu wote shuleni hapo alimshukuru Mkuu wa shule kwa kuona Umuhimu wa kuwa na jezi za michezo, na kuahidi kuwa shule hiyo itafanya vizuri katika mashindano ya UMISSETA kwa mwaka 2025/26.

Katika picha wakwanza kutoka kushoto ni Ntarisa K. Ntarisa (Mkuu wa shule ya sekondari Mndumbwe), Issa Lyoka (kiranja wa michezo Mndumbwe sekondari),Shani Bakari (kiranja wa michezo) na Mwansite W. Shali (Mwalimu wa michezo Mndumbwe sekondari) wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo. 

Kwa niaba ya Wanafunzi wote, viranja wa michezo katika shule hiyo walimshukuru Mkuu wa shule yao Mwalimu Ntarisa K. Ntarisa kwa kusema kuwa watajitahidi kwa kadri ya uwezo wao na kuwahamasisha Wanafunzi wenzao kufanya vizuri si katika michezo tu bali hata katika ufaulu wa masomo darasani.

Viranja wa michezo shule ya sekondari Mndumbwe, katikati ni Issa Lyoka, kushoto kwake ni Shani Bakari na kulia kwake ni Asma Abilah

Shule ya sekondari Mndumbwe inamandhari mazuri yanayo wezesha walimu kufundisha na Wanafunzi kujifunza, kwani shule hiyo inao walimu wenye weledi wanaojituma kufanya kazi na wanaozingatia ufundishaji wa kutumia zana za ujifunzaji hali inayopelekea Wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao ya ndani na nje ya shule 

Mwalimu Mathayo M. Kwaslema, Mwalimu wa somo la Biology akifundisha darasani, pembeni yake ni mwanafunzi wake akimskiliza kwa makini. 


Mwalimu Mathayo M. Kwaslema akiwa darasani akifundisha somo la Biology, kulia kwake ni Wanafunzi wakiwa wameshika zana za kujifunzia. 


Wanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Mndumbwe wilayani Tandahimba mkoani Mtwara wakiwa darasani wakijifunza

Wanafunzi wakimsikiliza Mwalimu wao wa somo la Biology Mathayo M. Kwaslema akifundisha kwa vitendo na kutumia zana. 


Mwisho 

Post a Comment

0 Comments